Jumatano, 17 Julai 2013

Waimbaji mbalimbali wakitoa burudani katika Mkutano kkkt Mbalizi mbeya














































MAHUBIRI SEHEMU YA PILI



MAONO NA GIZA(VISION AND DARKNESS)
Mwanzo 15:12(Na jua lilipokuwa likichwa usingizi mzito ulimshika Abrahamu hofu ya giza kuu ikamwangukia)Jina Abramu mana yake Baba aliyetukuka(exoted father)aliteuliwa na Mungu akatolewa katika jamaa zake na mila za kwao nae Jehova akampatia maono ya kuwa Baba wa mataifa mengi,wakati huo mke wake ni tasa lakini Mungu  anampa  ahadi ya kuwa taifa kwa Agano,elewa kwamba kila Agano huwa lina alama zake,katika agano hili alipewa alama ya kuchinja wanyama ya sadaka wa miaka mitatu mitatu na kumbuka kwamba kila namba ina mana yake,namba tatu inawakilisha ufufuo Mungu akionyesha anavyoenda kufufua maisha yake tena,Mungu akithibitisha kurejesha matumaini iwapo atadumu katika imani na kumtumainia Mungu.
Mungu anapompa mteule wake maono anamweka katika mikono yake akiwa pale katika uvuli wa mikono yake kuna giza lijalo,kutokana na utukufu wa mikono yake(In the brighteness of His hand)lipo giza kwa sababu ya excess of light,kwa hiyo kazi ya mteule ni kuwa pale katika mikono ya Mungu na kusikiliza,katika utukufu wa Mungu kwa ajili ya ule mng’ao macho ya mteule hutiwa kiwi 1Tim 6:16 kwa sababu nuru yake haiwezi kukaribiwa ukiutazama utukufu wake macho yako yanatiwa upofu,ndio maana ukisema unaona katika utukufu wa Mungu upo upofu,na ukiusogelea huo utukufu wa Mungu ukiwa kipofu ndipo unapotiwa nuru,hebu jifunze  kutulia mbele za Mungu na kusikiliza Mwanzo 16:2 -4 Abrahamu aliondoa usikivu wake kwa MUNGU akaweka kwa mke wake baada ya giza la maono aliyompatia kuchelewa,Mungu hawahi wala hachelewi hufanya kila kitu kwa wakati wake ukiwa mtulivu ukitambua kwamba Mungu akikupa maono na giza linafuatilia maono hayo ondoa hofu ya giza isikutishe na kuzuia usikivu wako kwa Mungu wakati wa giza hata ushauri unaweza ukakupoteza
Katika somo hili tunamwona Abramu akipewa ahadi ya kuwa taifa akimrudishia matumaini yaliyopotea hata kufungua mlango wa kuleta Ishmael ,desturi ya agano wakati ule wanyama wakichinjwa ambao ni wa agano hupasuliwa kati na wale wafanyao agano hupita katikati ya vipande vile,wakivitambuka ambayo ni alama ya kukubali kwamba kifo kilichowapata wanyama wale kiwapate wao iwapo watavunja ahadi ya agano lao,kwa hiyo Mungu alimwagiza Abramu awaandae wanyama wa agano Mwanzo 15:7-11.Mungu peke yake kwa mfano wa moto wa tanuru na moshi alipita katikati ya vipande vile maana peke yake alichukua madaraka ya kutimiza ahadi za agano lile hapo ndipo tunaiona neema ya Mungu ilivyo ya ajabu nae Abramu akayapokea kwa imani,lakini hata hivyo alikuwa na hofu ya giza wakati jua limekuchwa
Kuchwa kwa jua maana yake ni vipindi vya mashaka,vipindi vya wasiwasi na hofu,vipindi vya kukatishwa tamaa na kuvunjwa  moyo labda kwa sababu ya umri hivyo vyote havimzui Mungu kutimiza ahadi yake yeye asemi uongo Ebr 6:18(Ili kwa vitu viwili visivyoweza kubadilika ambavyo katika hivyo Mungu hawezi kusema uongo,tupate faraja iliyoimara sisi tuliyokimbilia kuyasika matumaini yale yawekwayo mbele yetu)haijalishi kuwa jua linakuchwa uaminifu wa Mungu uwe ndio ngao yetu,Yer 1:12 Mungu yuko makini kwa ahadi zake,amini tu agano lake hutimizwa wakati wa upinzani mkubwa,hutimizwa wakati wa utumwa,hukumu na kunyanyashwa kwa muda bado Mungu ni mwaminifu huonyesha uvumilivu wake kwa watu wa Kaanani ili kuwapa nafasi ya kutosha wapate toba lakini baada ya uovu wao kuzidi,unyanyasaji wao kuzidi,upinzani wao kuzidi maangamizo yao wakaanani yanakuja tu,Israeli lazima wapite maana ni ahadi ya Mungu kurithi Nchi.Watu wa imani lazima kushiriki Baraka zilizoahidiwa   bila kuogopa upinzani uliopo katika maisha ahadi ya raha ya sabato yaja anayeitoa ni Jehova asiyesema uongo,akikupa maono giza linafuata usiogope tulia tuli ukimsikiliza katika uvuli wa mikono yak,ni hatari kwako wakati wa giza kusikiliza ushauri mzuri badala ya kusubiri Mungu alete nuru hata wenye hekima wanaweza kukpoteza usijaribu kumsaidia Mungu kutimiza neno lake.Abramu alipitia miaka kumi na tatu ya ukimya(thirteen years)namba ya ukimya namba ya ukimya na mashaka,wakati ambapo wawezza kuharibu mema yote usipotulia katika uvuli wa mikono yake,kipindi cha ukimya ni kipindi cha nidhamu sio hamaki na presha,usilazimishe furaha na ujasiri bali bali kwa Mungu na ahadi zake vinginevyo utamleta Ishmael wewe na itakuwa mwanzo wa usumbufu Isaya 50:10-11(Ni nani miongoni mwenu amchaye Bwana,akiitiiye sauti ya mtumishi wake?)Sauti ya mtumishi ni zaidi ya andiko,ni elekezo la kinabii
Yeye aendae katika giza wala hana nuru nae alitumainia jina la Bwana na kumtegemea Mungu wake,Tazama ninyi nyote muashao moto na kujifungia hiyo mienge,enendeni ninyi katika mwale wa Moto wenu na katikati ya mienge mliyoiwasha matayapata haya kwa mkono wangu mtalala kwa huzuni
Tuache ushauri wa wenye hekima za dunia wakati tunalo neon la ahadi ya Mungu,huko ndiko kujiwashia moto utakaotuteketeza wenyewe na kuharibu mfumo ambao Mungu ameuweka,uwe mvumilivu ili upate ahadi ,usiue maono yako kwa kusukiliza mashauri ya watu na hofu za giza Mungu ni mkweli hasemi uongo bado yapo matumaini kwa walionyanyaswa na kuonewa,bado lipo tumaini kwa walioteswa na ibilisi na magonjwa,bado lipo tumaini kwa Tanzania.Amini tu na subiri kwa matumaini yeye ajaye atakuja wala hatakawia
                       Barikiwa
                                     Yohana kangajaka
Kwa mawasiliano zaidi ya kihuduma au maoni na maombezi wasiliana nae kwa simu namba  +255 758 456 221 au ukipenda kuwezesha Huduma kwa M-pesa.Karibu na Mungu atakubariki
                                    Imechapiswa na Baraka Msele