Mafundisho Na Semina

LAWI 26:13
“Mimi ndimi Mwenyezi Mungu wenu niliyewatoa nchini Misri ili msiwe watumwa wa Misri.Mimi nimevinja nira mliofungiwa shingoni mwenu na kuwafanya mtembee wima.”
Mungu ansema wewe umefungiwa nira,wewe ni mtumwa,unafanya mambo kwa faida yaw engine ni mtumwa,naye Mungu hataki uwe mtumwa wa watu,una utumwa flani huwezi kuifungua mwenyewe.Umetekwa na ushirikina wewe huwezi fanya jambo bila kupitia kwa waganga wewe mtumwa,wewe mchawi mtumwa,kila wakati umetamani uache lakini huwezi wewe,mtumwa wa pombe,mtumwa wa sigara,mtumwa wa ngono,mtumwa ugomvi hukuacha mahali usigombane,wewe mzuushi umezuwa mengi ni mtumwa sikia…….Mwenyezi Mungu anasema asemacho Anayo nguvu ya kuvunja hiyo Nira uliyofungiwa shingoni.Imeinamisha chini maisha yako,umepinda wewe.
Bwana anasema tembea wima sasa,tembea sawasawa wima,umeubwa utembee wima si kama mnyama,umepindishwa na kitu gani kinachokufanya uwe na chuki na wengine?Wewe mbona unafnaya vitu vya kinyama umepinda hakuna wa kukufanya utembe wima basil Mungu aliyekuumba.”Sikia ujumbe huu,acha kuwa kibaraka wa watu au wa shetani.NJOO KWA MKOMBOZI AKUFUNGUE LEO
Mwana akiwaweka huru mtakuwa huru kwelikweli Yn 8:36() na 10:4.Fuata sauti ya Roho wa Bwana kutolewa katika kifungo chochote ni zaidi ya kuombewa.Biblia hapa haijasema swala la maombi bali Yn8:32()kweli inafungua .Tena anasema akikutoa nje atakutangulia nawe ufuate kwa kujua sauti yake.Neno la kinabii lawez akutoka kwa ajili yako ndilo ulifuate hajasema wanajua andiko bali  amesemea sauti
UPAKO
Wakati huo mzigo walowabebesha nitamumuondoa na Nira waliowatia shingoni mwenu itavunjiwa.Upo upako wa mafuta ya Uhuru yanayopatikana kwa wale wanaofanya muda wao kwa maombi katika Roho Mtakatifu,wako watu hawajui kuwa maombi yanafanya barabara ya mafuta ya Roho wa Yesu ili kusafisha hali ya Hewa na Mungu kutenda miugiza.shida nyingi watu hawaombi….kazi  yao ni manunguniko ,maneno maneno lakini ukiomba na kumruhusu Roho wa maombi utayavuta mafuta ya upako na maisha ya wengi yangebadilika.na Hata nchi Yetu ingebadilika,Wakorofi wangeshughulikiwa na mafuta wakatubu.
Upo uhuru katika upako wa mafuta ukiomba katika Roho.Anza kujitoa ukiruhusu upako uje maishani mwako.Nira itavujwa wakati huo unao msingi katika kwelu ya Neno la Mungu ambalo neno lakupa ufahamu katika maarifa ya Kimungu yani “DIVINE KNOWLEDGE”.Mungu alipomchagua mtu kati ya watu wa mataifa yote duniani ili anzishe Taifa jipya kuwa chombo cha kupeleka Baraka zake kwa Mataifa yote Mwanzo 12:2—3,mtu huyu alikuwa mteule wa Mungu naye ni Abramu ambaye baadaye aliitwa Ibrahimu.Awali huyu aliishi kwa waabudu sanamu wa wakaldayo (Babeli ya kale)Yosh 24:2.Abramu almtii Mungu hakutembea na roho ya ukoo,alitii alipoamriwa kuhama na walihama Mungu alipowaamuru kuhama hadi kanaani.
Hakukua na kizuizi cha uzee au utasa Mwanzo 12:15(),Ebra 11:8—12,Abramu alionyesha Heshima yake alipojenga madhabahu katikati ya mako ya wakaanani Mwanzo 12:6—9,mtu huyu aliongozwa na Mungu naye Mungu akamuongeza na zilikwepo ahadi saba
·        Taifa kubwa
·        Kubarikiwa
·        Kulikuza jina lako
·        Kuwa Baraka
·        Wanaokubariki watabarikiwa
·        Wanaokulaani watalaaniwa
·        Kupitia wewe wengi watabarikiwa
 





Moja kati ya Semina na Mafundisho juu ya Unabii na Nabii KKKT Usharika wa Makorora Tanga ambayo ilifanyika kwa Mabinti Sayuni









BWANA YESU ASIFIWE TUNAPENDA KUWAKARIBISHA KATIKA SOMO  LETU TENA
SOMO LA LEO LINAHUSU MAVUNO.yeremia 8:18-20
Mavuno yamepita wakati wa hali umekwisha walasisi hatukuokoka Nabii anaonyesha huzuni kubwa ya dhambi na uharibufu wa watu wa Mungu.

yeremia 8:18 inasema laiti ningeweza kujifariji nisione huzuni .Moyo wangu umezimia ndani yangu. Tazana sauti ya kilio cha binti ya watu wangu ,itokayo katika nchi iliyo mbali sana,Je! BWANA hayumo katika sayuni? M felme wake hayumo ndani yake? mbona eamekasirisha kwa sanamu zao walizochonga na kwa ubatili wa kigeni? Nabii anavutwa kati ya uaminifu wake na mungu nauhusiano wake na watu yuko katika uchungu mkali mnokiasi kwamba anataka kujitenga na hao watu.Watu wa mungu wanapiti aina hii ya huzunu
wanapowaona watu wanao wapenda wakiishi kinyume na mapenzi ya mungu wakifanya uasi dhidi ya mungu na njia zake za haki.Kwasababu watumishi wa bwana mungu ni wawakilishi wa mungu wanapitia huzuni ya mungu akiona watu wake wakiishi kinyume na mpango wake au  kinyume na kanuni za utawala wake mbele yao kuna janga linalo wasubiri wote wasio na toba bila kujali wanatoka dini gani wanacheo gani au hawana cheo ndio maana nabii anaonyesha majuto kwamaana mungu hafurahii kifo cha mwenye dhambi ndio maana moyo wake unahuzuni amtazamapo muasi ndiosabababu Nabii anaonyesha majuto akisema mavuno yamepita wakati wa hali umekwisha haya ni manena ya kujuta (waswahili wanasema majuto ni mjukuu) Mpendwa wangu usomae ujumbe huu ni mombi yangu usiwe miongoni mwa hao watakao jutia maisha yaiyo pita Mungu anakupenda hataki ufe katika dhambi usomapo ujumbe huu mfupi fanya maamuzi leo uje katika toba na kuiamini kazi ya mungu katika Yesu kristo nawe huta juta.Mavuno ni alama ya ukomavu wa jambo linalo lea matokeo elewa dhambi inaanzia kwenye tamaa mbaya tamaa ikisha komaa inaza mauti matokeo  ni
 uharbifu wa mwili na roho usikiapo sauti hii usifanye moyo wako kuwa mgumu unaweza kuungana nami katika ala hii ya toba na kumpa yesu maisha yako (sema baba Mungu ninakushuru kwasababu wewe upendo wako hauna mipaka unanipenda ha mimi mwenye dhambi na unichukia dhambi kuanzia sasa kupitia ujumbe huu nageuka na kutubu nisamehe dhambi zangu zote futa jina langu katika kitabu cha hukumu na uliandike kwa upya katika kitabu cha uzima niaikubali damu ya Yesu kwamba imeninunua kuanzia sasa mimi ni mali yako mungu katika jina la Yesu amina) kama umesali sala hii kwa imani amini kwamba umeokoka tafut watu wanao mwamini Yesu kama mwokozi wao jifuze jinsi ya kuukulia wokovu ka unadwali wasiliana nasi kwa simu namba+255758456221.


*********************************************************************************


my people are distroyed for luck of knowledge.hosea4:6
watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa.
Maarifa ni ELimu tupatayo . vyanzo vyake ni pale ulipozaliwa watu wakuzungukao,shule tusomazo.vyote ni vyanzo vya maarifa..mimi leo nazungumzia maarifa yakiMUNGU;DIVINE KNOWLEDGE.nabii Isaya11:2Na ROHO WA BWANA.atakaa juu yake .Roho ya hekima na ufahamu Roho wa shauri na uweza. Roho ya maarifa na ya kumcha Bwana,
ni moja ya roho saba za MUNGU Maarifa ni roho kama vile Imani;2kor4:13Lakini kwakua tuna roho ileile ya Imani,kama ilivyoandikwa naliamini na kwasababu hiyo nalinena. sisi nasi twaamini na kwasababu hiyo twanena'hapa huonyesha wazi kwamba Imani ni roho.roho huwa haifi mwili ndio hufa ndio maana mtu wa Imani hazuiliwi na kitu nabii Yeremia2:21-24Nami nalikuwa nimelipanda, mzabibu mwema sana, mbegu nzuri kabisa umegeukaje basi kuwa mche usiofaa wamzabibu mwitu machoni pangu? maana ujapo jioosha kwa magadi ,nakujipatia sabuni ni nyingi lakini uovu wao  umeandikwa mbele zangu,asema Bwana MUNGU.Wawezaje kusema sikutiwa unajisi, sikuwafuata mabaali?Itaza me njia yako bondeni,ujue uliyoyatende ,weweya unga mia mwepesi apitaye katik a njia ake.israel ilimwacha Mungu wakiaishi maisha yao yasiyo mpendeza Mungu maisha nje na kusudi la  Mungu kwa kukosa maarifa kwao Muerengu amkamtuma Yeremia yeremia  4:22 kwa maaana  watu  wangu niwaa pumbavu , hawajui ni watoto walio pungukiwa na akili wala hawana ufahamu ,ni wenye akili katika kutenda mabaya bali katika kayutenda
mema hawana maarifa.
1 GNOSS: UJUZI Elimu ya  shule itakayokufanya ujue sayansi , nakufanya mkristo wa kawaida kuwa na Mungu na kufa.
2 GNOSKO Elimu ya ufunuo ya mtu ambaye anaelewa Neno kwa ku sikia :ibada ,semina mkutano lakini siye msomaji wa Neno la Mungu hana hofu ya Mungu yeremia 5:4Ndipo nikasema,Hakika hawa ni maskini ,ni wajinga hawa maana hawajui njia ya Bwana,wala hukumu ya Mungu wao.ana cheo kanisani serikali.

Hakuna maoni: