Ijumaa, 20 Septemba 2013



Mtumishi wa Mungu Yohana Kangajaka




Waimbaji Wakimsifu Mungu

Waimbaji wakimsifu Mungu katika mkutano wa injili



Wanafunzi wa shule ya Uhuru

Wanafunzi wa shule ya msingi UHURU wakifuatilia  Neno la Mungu katikt  mkutano

Akitumbuiza kwa shangwe

Mwimbaji akimtukuza Mungu wakati wa mkutano wa injili mjini Makambako

Watoto wakifatilia maombezi

Mungu aliseama waacheni watoto wadogo waje kwangu, kwa maana ufalme wa mungu niwao na pia akasema afananae na mtoto huyu ufalme wa mungu u juu yake hawa ni watoto waliopendezwa na mungu wakajaaliwa kushiriki katika mkutano wa injili uliokua ukiongozwa na Mtumishi wa Mungu Yohana Kangajaka.

makutano wakisikiliza mahubiri

Wengi wao waliokoka wengine waliokolewa katika vifungo vyao na mateso ya ibilisi shetani ushuhuda ulitolewa kwa watu mbalimbali wanawake wengi wakiijua kweli ya MUNGU nao walikombolewa.

MAVUNO.yeremia 8:18-20

BWANA YESU ASIFIWE TUNAPENDA KUWAKARIBISHA KATIKA SOMO  LETU TENA
SOMO LA LEO LINAHUSU MAVUNO.yeremia 8:18-20
Mavuno yamepita wakati wa hali umekwisha walasisi hatukuokoka Nabii anaonyesha huzuni kubwa ya dhambi na uharibufu wa watu wa Mungu.

yeremia 8:18 inasema laiti ningeweza kujifariji nisione huzuni .Moyo wangu umezimia ndani yangu. Tazana sauti ya kilio cha binti ya watu wangu ,itokayo katika nchi iliyo mbali sana,Je! BWANA hayumo katika sayuni? M felme wake hayumo ndani yake? mbona eamekasirisha kwa sanamu zao walizochonga na kwa ubatili wa kigeni? Nabii anavutwa kati ya uaminifu wake na mungu nauhusiano wake na watu yuko katika uchungu mkali mnokiasi kwamba anataka kujitenga na hao watu.Watu wa mungu wanapiti aina hii ya huzunu
wanapowaona watu wanao wapenda wakiishi kinyume na mapenzi ya mungu wakifanya uasi dhidi ya mungu na njia zake za haki.Kwasababu watumishi wa bwana mungu ni wawakilishi wa mungu wanapitia huzuni ya mungu akiona watu wake wakiishi kinyume na mpango wake au  kinyume na kanuni za utawala wake mbele yao kuna janga linalo wasubiri wote wasio na toba bila kujali wanatoka dini gani wanacheo gani au hawana cheo ndio maana nabii anaonyesha majuto kwamaana mungu hafurahii kifo cha mwenye dhambi ndio maana moyo wake unahuzuni amtazamapo muasi ndiosabababu Nabii anaonyesha majuto akisema mavuno yamepita wakati wa hali umekwisha haya ni manena ya kujuta (waswahili wanasema majuto ni mjukuu) Mpendwa wangu usomae ujumbe huu ni mombi yangu usiwe miongoni mwa hao watakao jutia maisha yaiyo pita Mungu anakupenda hataki ufe katika dhambi usomapo ujumbe huu mfupi fanya maamuzi leo uje katika toba na kuiamini kazi ya mungu katika Yesu kristo nawe huta juta.Mavuno ni alama ya ukomavu wa jambo linalo lea matokeo elewa dhambi inaanzia kwenye tamaa mbaya tamaa ikisha komaa inaza mauti matokeo  ni
 uharbifu wa mwili na roho usikiapo sauti hii usifanye moyo wako kuwa mgumu unaweza kuungana nami katika ala hii ya toba na kumpa yesu maisha yako (sema baba Mungu ninakushuru kwasababu wewe upendo wako hauna mipaka unanipenda ha mimi mwenye dhambi na unichukia dhambi kuanzia sasa kupitia ujumbe huu nageuka na kutubu nisamehe dhambi zangu zote futa jina langu katika kitabu cha hukumu na uliandike kwa upya katika kitabu cha uzima niaikubali damu ya Yesu kwamba imeninunua kuanzia sasa mimi ni mali yako mungu katika jina la Yesu amina) kama umesali sala hii kwa imani amini kwamba umeokoka tafut watu wanao mwamini Yesu kama mwokozi wao jifuze jinsi ya kuukulia wokovu ka unadwali wasiliana nasi kwa simu namba+255758456221. 
Mtumishi wa Mungu akiwa anafanya huduma katika mkutano mjini Makambako
wanakwaya wa Amani gospel Mbeya wakimsifu katika mkutano wa injil mjini Makambako