Alhamisi, 19 Desemba 2013

MATHAYO ALIITWA NA BWANA

MATHAYO ALIITWA NA BWANA

Mt 9:9--13(Naye Yesu alipokuwa akipita kutoka huko aliona mtu ameketi forodhani aitwaye Mathayo,akamwambia,nifuate.Akaondoka akamfuata.10 Ikawa alipoketi nyumbani ale chakula,tazama,watoza ushuru wengi na wenye dhambi walikuja wakaketi pamoja na Yesu na wanafunzi wake.11 Mafarisayo walipoona hayo waliwaambia wanafunzi wake,mbona mwalimu wenu anakula na kunywa pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi?12 Naye aliposikia aliwaambia,Wenye afya hawahitaji tabibu bali walio hawawezi.13 Lakini nendeni,mkajifunze maana yake maneno haya,nataka rehema wala si sadaka;kwa maana sikuja kuwaita wenye haki bali wenye dhambi.)

Nifuate akaondoka akamfuata,mzigo wa Yesu na maono yake yakawa maana ya mathayo.Mathayo ameongezwa katika kundi la wanafunzi wa Yesu,ameteuliwa naye akaondoka katika mazoea ya dhambi,akamfuata yaani akafanya yale Yesu afanyayo,hakufuata tabia za watoza ushuru wengine wala tabia za jina lake la kale.Ndipo alivyoona wema wa Yesu alimualika nyumbani kwake na kumpa Yesu chakula.Chakula cha Yesu ni kufanya mapenzi ya baba yake,mathayo alialika watoza ushuru wengine ili wakutane na Yesu alijua sasa mafanikio anayo Bwana mpya Bosi wa maisha yake,alitaka marafiki wamwone.

Wakati huo wayahudi walikuwa wandharau sana watoza ushuru waliwaona kuwa katika taifa lao ni watu wasio na dini,watu wadanganyifu ,walipomwona Yesu yupo pamoja na katika mlo wakamdharau na Yesu (Mt 9:10—11) ukisoma Luka 5:27—30(Baada ya hayo akatoka akaona mtoza ushuru,jina lake Lawi,ameketi forodhani,………………………………………………………….)Yesu alijibu hoja zao,akawaambia kama hawa watoza ushuru ni wabaya ndio hasa walaohitaji msaada wake.

Mbingu zilikuwa pamoja na Yesu,Mungu Baba alipendezwa na Tendo la Pendo na neema kwa watu waliotengwa na ushirika wa jamii.Mungu hapendezwi na sadaka za watu wanaojidai kuwa ni wema kuliko wengine,hebu tambua thamani yako anayo jehova tu.Acha vyote mfuate utaona utukufu wake nawe utakuwa chombo,acha dhambi,wengi watanona utukufu wake.Amina

ENDELEA KUFUATILIA HABARI MBALIMBALI KWENYE BLOG YETU UPATE KISA CHA MALKIA WA KUZIMU ALIVYOTAKA KUMSHAMBULIA MTUMISHI WA MUNGU YOHANA KANGAJAKA NA UELEWE JINSI GANI WANAFANYA KAZI ZAO KUPINGA KAZI ZA MUNGU

Tunaendelea kuwakaribisha katika Semina tena siku ya leo ndani ya viwanja vya KKKT Usharika wa Handeni
MHUBIRI;GRACE MPANDUJI
SOMO;NYAKATI ZA HATARI
2TIMOTHEO 3:1
(Lakini ufahamu neno hili,ya kuwa siku za mwishokutakuwako nyakati za hatari.2 maana watakuwa wa kujipenda wenyewe,wenye kupenda fedha,wenye kujisifu,wenye kiburi,wenye kutukana,wasiotii wazazi wao,wasio na shukrani,wasio safi.3 wasiowapenda wakwao,wasio taka kufanya suluhu,wasingiziaji,wasiojizuia,wakali,wasiopenda mema.4 Wasaliti,wakaidi,wenye kujivuna,wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu ;5 wenye mfano wa utauwa,lakini wakikana nguvu zake,hao nao jiepushe nao.) 

ENDELEA KUFUATILIA KUPITIA YOUTUBE @ http://www.youtube.com/channel/UCNQi8Dm-n98w671gUKbpiew/videos   NA FACEBOOK PAGE @https://www.facebook.com/yohana.kangajaka.3

WEBSITES :WWW.KANGAJAKA.COM

NYAKATI ZA HATARI