Alhamisi, 24 Septemba 2015

Extraordinary Invitation (Mwaliko usio wa kawaida) By Yohana Kangajaka



 Extraordinary Invitation

(Mwaliko usio wa kawaida)



 John 7:37 john 4:10,14 ikor 10:4 and exodus 16:4, 14-15, 17:6

Chota katika kisima cha uzima, maneno haya yanamaanisha viko visima vingi, lakini fahamu vingine vina maji machungu yanayoleta uchungu na uharibifu. Kuna kisima kimoja cha pekee chenye maji ya uzima, maji yaburudishayo jangwani na mwamba huu ulioko jangwani jina lake ni Kristo Yesu wakati umekata tamaa hilo ni jangwa lako wakati umevunjika moyo,unachohitaji ni macho yaonayo ili uone hiki kisima cha chemichemi ya amani,furaha,kitakupa  changamko na afya kamwe ukipata maji haya hutazimia jangwani utapata nguvu mpya “you will not faint”

Ukiwa na roho ya kujiona hapo ni vigumu kupata haya maji na ni vigumu kupata muugiza wako lakini chemichemi ya maji katika mwamba ndio pekee yenye maji safi na hilo tatizo ulilonalo lipo katika mtazamo,nia safi ni muhimu iwapo unataka kupokea muugiza wako na umtukuze Mungu. Kabla ya kuchota maji jihoji kwanza ili usije chota katika chombo kichafu mithali 4:23 (watch over you heart with all diligence for from it flow the spring of life) Je unalinda nini? Dini yako? Mumeo,mkeo,mwanao utajiri wake,heshima yako,hebu litende haki neno la Mungu ili uone maajabu ya mwamba wa jangwani.

Kiriba chako cha maji kiunganishe na jabali ili uone wokovu katika afya yako,biasahra yako,elimu yako, maneno usemayo yatawaburudisha wengine na kuwaletea afya,moyo wenye uzaima wa Mungu mwenyezi Mith 14:30

Hutawajeruhi wengine kama panga na mishale ya sumu maana umeinua karama ya Mungu  umeyaomba maji toka mwaruba wa milele maana moyo una uhusiano wa karibu na mdomo, moyo ukiugua unahataridha maisha yako unaweza hata kufa kabla ya wakati wako chota leo mith 12:18 kabla hujaongea fikiri kwanza ,

Moyo unauwezo wa kuamua litakalotokea katika mwili,moyo wenye amani huleta uzima kwa mwili,linda sana moyo wako.Acha kuozesha mifupa kwa husuda na mashindano. Mith 18:14 stahihi tunza stawisha,lisha beba, inua,linda,saidia,tetea mwili wako na kuupatia mahitaji muhimu kwa ajili ya kuishi roho yako yakibinadamu itaweza kubeba na kulinda,kutunza mwili wako uwe na afya bila kujali hali mbaya unazokutana nazo roho yako inaweza na ukaendelea kuishi maana umeunganisha kiriba chako na mwamba wa chemichemi ya uzima hivyo nia ya kuishi inakutegemeza mara utakapokuwa mgonjwa maana roho yako ina uzima ndio itasambaza uzima katika mwili wako pia

Lakini ukipoteza tumaini lako hata ukioombewa unajisumbua tu. Nia ya kuishi lazima itoweke kamwe usiondoke katika imani yako wala katika ahadi za maisha marefu nia ya kuishi ndio inayoweza kumtegemeza mwamini hata atakapotishwa na magonjwa yasiyotibika kama nia ipo na njia ya kuishi ipo itasimamisha usalama.Ponya roho kwanzana roho itaponya mwili Mith 17:22 nilile neno la Mungu lililopo mdomoni mwetu ndilo huponya roho Rum 7:22, 2kor 4:16

Acha utu wa ndani ufanywe upya utu wa nje utaongozwa toka ndani  Yer 29:13 mtafute huyu mwamba jijaribu mwenyewe 2kor 13:5 na ujiweke wakfu mwenyewe Yn 17:19 na 1yn 1:8-9    this is the message we have from Him and proclaim to you, that God is light and in Him there is no darkness at you  1 Yn 1:7

                                                                                                                        posted by @bless msele