Ijumaa, 5 Julai 2013
SOMO
NIDHAMU YA KUSIKILIZA
The
discipline of heeding Math 10:27 (Nawaambieni ninyi kkatika giza lisemeni katika nuru na msikialo kwa
siri lihubirini juu ya nyumba.
Kumbe ziko nyakati ambazo
Mungu anatuweka katika nidhamu katika giza na hutufundisha kumsikiliza
yeye.Viko vitu vingi hutujia ili tuvisikilize lakini katika giza jifunze
kutulia katika mikono ya Mungu aliye hai na kuimba sifa zake wala sio kuongea
giza lako ili ubakie katika uvuli wa mikono ya Jehova hata utakapo jifunza
kusikiliza na kusikiliza sauti yake isemayo katika giza anasema niwaambialo
ninyi katika giza,kumbe katikati ya giza lolote maana yake katikati ya mambo
tusiyo yaelewa ruhusu yule asiyeonekana ili atoe sauti yake inayoweka ufahamu
ndani yetu.Haki sasa pengine umezungukwa na mambo huyafahamu hata sababu zake
kwanini yanayokupata na unawaza kwanini wewe.Iwapo wewe ni mkristo wa kweli
zingatia hili,Yesu anaongea na wanafunzi wake,watu wale waliotayari kujifunza
kwake na kuchukua nira yake na utayari wa kujifunza kwake hata wakati ambao ni
wa giza,wakati wa giza ni wakati wa hofu,wakati wa mashaka giza kiafya giza
kiuchumi giza pande zote usiruhusu hofu amini uwepo wa Bwana.
Mungu ana,pokuweka katika giza na
unapokuwa pale katika giza funga mdomo wako ili usije ukakamatwa kwa maneno ya
kinywa chako “keep your mouth shut”when your in dark.Pengine ndivyo sasa ulivyo
upo katika utata wa maisha na maamuzi yako hayaeleweki tulia na jifunze kuto
kusemasema ili umuache Mungu aseme,ukifungua kinywa wakati wa giza utaongea
vibaya in the wrong mood.Gizani kipindi cha kusikiliza sio kipindi cha
kusema,kutokusema sio alama ya kutokujua bali ni adabu ya yeye aonaye
gizani,giza halimfichi kitu ukimpa nafasi ukimheshimu na kukaa kimya
utamhusisha yeye atamke akitamka neno juu yako neno lake litaumba muujuza
wako.Acha kusema na watu juu ya giza lako acha kutafuta sababu za giza kwa
wenye hekima na marafiki bali sikiliza Jehova
asemaye katika giza.Ukizungumza na watu hutasikia yale Mungu asemayo
utagonganisha maneno ya watu na Mungu na hiyo sio nidhamu ,wewe uwe na nidhamu
ya kumsikiliza Mungu ukiwa katika giza
ya yale yakuzungukayo usikivu wako wakati wa giza utakupatia ushuhuda wa
thamani sana wakati ukitokea nuruni.Baada a vipindi vya giza huja na vitu mchanganyiko
na hofu yenye furaha ndani yake utashangaa mbona ulikuwa huelewi japo ulikuwa
unasikia hali hizo,elewa ni majira Mungu ameweka ufahamu na karama ya
unyenyekevu unaoleta moyo mnyofu ambao wakati wote utamsikia Mungu asemapo.
Mungu atuapatie nidhamu ya kusikiliza
na kukua katika maarifa ya mapenzi yake pokea ujasiri na usikivu wa Kiungu
wakati wa mambo magumu katika jamii,familia,hata Taifa pia tuelewe siku zote
sio Jumapili.Tujifunze nidhamu ya kusikiliza wala sio kusema.
Barikiwa Ev.Yohana Kangajaka Wasiliana nae kwa namba (+225758456221) or +2250715279702 kama ukitaka kusaidia Huduma.Mungu akubariki
Nyimbo
Moja kati ya nyimbo za Yohana kangajaka karibu katika Albamu Nasonga mbele kwa Mawasiliano zaidi wasiliana nae kwa simu No. +255758456221
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)