Jumatano, 17 Julai 2013
MAHUBIRI SEHEMU YA PILI
MAONO
NA GIZA(VISION AND DARKNESS)
Mwanzo
15:12(Na jua lilipokuwa likichwa usingizi mzito ulimshika Abrahamu hofu ya giza
kuu ikamwangukia)Jina Abramu mana yake Baba aliyetukuka(exoted
father)aliteuliwa na Mungu akatolewa katika jamaa zake na mila za kwao nae
Jehova akampatia maono ya kuwa Baba wa mataifa mengi,wakati huo mke wake ni
tasa lakini Mungu anampa ahadi ya kuwa taifa kwa Agano,elewa kwamba
kila Agano huwa lina alama zake,katika agano hili alipewa alama ya kuchinja
wanyama ya sadaka wa miaka mitatu mitatu na kumbuka kwamba kila namba ina mana
yake,namba tatu inawakilisha ufufuo Mungu akionyesha anavyoenda kufufua maisha
yake tena,Mungu akithibitisha kurejesha matumaini iwapo atadumu katika imani na
kumtumainia Mungu.
Mungu
anapompa mteule wake maono anamweka katika mikono yake akiwa pale katika uvuli
wa mikono yake kuna giza lijalo,kutokana na utukufu wa mikono yake(In the
brighteness of His hand)lipo giza kwa sababu ya excess of light,kwa hiyo kazi
ya mteule ni kuwa pale katika mikono ya Mungu na kusikiliza,katika utukufu wa
Mungu kwa ajili ya ule mng’ao macho ya mteule hutiwa kiwi 1Tim 6:16 kwa sababu
nuru yake haiwezi kukaribiwa ukiutazama utukufu wake macho yako yanatiwa
upofu,ndio maana ukisema unaona katika utukufu wa Mungu upo upofu,na ukiusogelea
huo utukufu wa Mungu ukiwa kipofu ndipo unapotiwa nuru,hebu jifunze kutulia mbele za Mungu na kusikiliza Mwanzo
16:2 -4 Abrahamu aliondoa usikivu wake kwa MUNGU akaweka kwa mke wake baada ya
giza la maono aliyompatia kuchelewa,Mungu hawahi wala hachelewi hufanya kila
kitu kwa wakati wake ukiwa mtulivu ukitambua kwamba Mungu akikupa maono na giza
linafuatilia maono hayo ondoa hofu ya giza isikutishe na kuzuia usikivu wako
kwa Mungu wakati wa giza hata ushauri unaweza ukakupoteza
Katika
somo hili tunamwona Abramu akipewa ahadi ya kuwa taifa akimrudishia matumaini
yaliyopotea hata kufungua mlango wa kuleta Ishmael ,desturi ya agano wakati ule
wanyama wakichinjwa ambao ni wa agano hupasuliwa kati na wale wafanyao agano
hupita katikati ya vipande vile,wakivitambuka ambayo ni alama ya kukubali
kwamba kifo kilichowapata wanyama wale kiwapate wao iwapo watavunja ahadi ya
agano lao,kwa hiyo Mungu alimwagiza Abramu awaandae wanyama wa agano Mwanzo
15:7-11.Mungu peke yake kwa mfano wa moto wa tanuru na moshi alipita katikati
ya vipande vile maana peke yake alichukua madaraka ya kutimiza ahadi za agano
lile hapo ndipo tunaiona neema ya Mungu ilivyo ya ajabu nae Abramu akayapokea
kwa imani,lakini hata hivyo alikuwa na hofu ya giza wakati jua limekuchwa
Kuchwa
kwa jua maana yake ni vipindi vya mashaka,vipindi vya wasiwasi na hofu,vipindi
vya kukatishwa tamaa na kuvunjwa moyo
labda kwa sababu ya umri hivyo vyote havimzui Mungu kutimiza ahadi yake yeye
asemi uongo Ebr 6:18(Ili kwa vitu viwili visivyoweza kubadilika ambavyo katika
hivyo Mungu hawezi kusema uongo,tupate faraja iliyoimara sisi tuliyokimbilia
kuyasika matumaini yale yawekwayo mbele yetu)haijalishi kuwa jua linakuchwa
uaminifu wa Mungu uwe ndio ngao yetu,Yer 1:12 Mungu yuko makini kwa ahadi
zake,amini tu agano lake hutimizwa wakati wa upinzani mkubwa,hutimizwa wakati
wa utumwa,hukumu na kunyanyashwa kwa muda bado Mungu ni mwaminifu huonyesha
uvumilivu wake kwa watu wa Kaanani ili kuwapa nafasi ya kutosha wapate toba
lakini baada ya uovu wao kuzidi,unyanyasaji wao kuzidi,upinzani wao kuzidi
maangamizo yao wakaanani yanakuja tu,Israeli lazima wapite maana ni ahadi ya
Mungu kurithi Nchi.Watu wa imani lazima kushiriki Baraka zilizoahidiwa bila
kuogopa upinzani uliopo katika maisha ahadi ya raha ya sabato yaja anayeitoa ni
Jehova asiyesema uongo,akikupa maono giza linafuata usiogope tulia tuli
ukimsikiliza katika uvuli wa mikono yak,ni hatari kwako wakati wa giza
kusikiliza ushauri mzuri badala ya kusubiri Mungu alete nuru hata wenye hekima
wanaweza kukpoteza usijaribu kumsaidia Mungu kutimiza neno lake.Abramu alipitia
miaka kumi na tatu ya ukimya(thirteen years)namba ya ukimya namba ya ukimya na
mashaka,wakati ambapo wawezza kuharibu mema yote usipotulia katika uvuli wa
mikono yake,kipindi cha ukimya ni kipindi cha nidhamu sio hamaki na
presha,usilazimishe furaha na ujasiri bali bali kwa Mungu na ahadi zake
vinginevyo utamleta Ishmael wewe na itakuwa mwanzo wa usumbufu Isaya 50:10-11(Ni
nani miongoni mwenu amchaye Bwana,akiitiiye sauti ya mtumishi wake?)Sauti ya
mtumishi ni zaidi ya andiko,ni elekezo la kinabii
Yeye
aendae katika giza wala hana nuru nae alitumainia jina la Bwana na kumtegemea
Mungu wake,Tazama ninyi nyote muashao moto na kujifungia hiyo mienge,enendeni
ninyi katika mwale wa Moto wenu na katikati ya mienge mliyoiwasha matayapata
haya kwa mkono wangu mtalala kwa huzuni
Tuache
ushauri wa wenye hekima za dunia wakati tunalo neon la ahadi ya Mungu,huko
ndiko kujiwashia moto utakaotuteketeza wenyewe na kuharibu mfumo ambao Mungu
ameuweka,uwe mvumilivu ili upate ahadi ,usiue maono yako kwa kusukiliza
mashauri ya watu na hofu za giza Mungu ni mkweli hasemi uongo bado yapo
matumaini kwa walionyanyaswa na kuonewa,bado lipo tumaini kwa walioteswa na
ibilisi na magonjwa,bado lipo tumaini kwa Tanzania.Amini tu na subiri kwa
matumaini yeye ajaye atakuja wala hatakawia
Barikiwa
Yohana kangajaka
Kwa
mawasiliano zaidi ya kihuduma au maoni na maombezi wasiliana nae kwa simu
namba +255 758 456 221 au ukipenda
kuwezesha Huduma kwa M-pesa.Karibu na Mungu atakubariki
Imechapiswa na Baraka Msele
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)