Alhamisi, 4 Julai 2013

NDOA NAFAMILIA ILIPOISHIA........


ILIPOISHIA NDOA NA FAMILIA
    Hakuna kuambatana iwapo roho ya ubinafsi imetenda kazi ukitaka kujenga urafiki wowote na mtu ujue kuna gharama lazima uwe na nia yenye nguvu ndani yako,lazima ukubali kuutumia muda wako,lazima ukubali kutumia nguvu zako na pia uwe mwaminifu,hakuna rafiki utakaye mpata aliye mkamilifu lakni uaminifu ni wa muhimu sana hata Mungu mwenyewe hawatumii watu wakamilifu bali anawatumia watu waaminifu.Ndani ya ndoa kunatakiwa uaminifu na sio ukamilifu kwa sababu ndoa ni agano asili yake ni Mungu na MUNGU ni muumbaji na ndoa ina sehemu ya uumbaji.Wakati mnashikana mikono mnatakiwa vidole kuingiliana kabisa ni alama ya utabiri ukitabiri kuambatana pamoja na alama ya uzao.uzao ni uumbaji Kiungu kupitia chembechembe za viuno vyen.Mtoto akiwa tumboni anakula kupitia kitovu cha mama yake hivyo wanaowana wakishikana  mikono kwa kuingiza vidole kila mmoja vikashonana hiyo ni ni spiritual symbolism ya kitovu cha mtoto kinavyoshonana na kitovu cha mama.Ambavyo hutabiri mwendelezo wa uumbaji lakini leo haifanyiki hivyo ndio sababu adui huanza kuingilia kuvuruga kutoshikamana,kumbuka Mungu alituumba kwa sura yake na mfano wake.Sifa ya Mungu:
a)Ni mwema hivyo kila chema kilichobarikiwa chenye upendo,chenye huruma na sadi ni cha MUNGU Yakobo 1:17.Pia Mungu anatoa uzima:Hawa jina lake lina maana ya uzima tena lina maana ya maisha kupitia viuno vyao maisha au uzima huendelezwa,Mtume petro anasema 2Petro 1:3 (Kwa kuwa uweza wake wa Uwungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe)na Dr luka nae amesema katika Luka 9:56 (For the son of man did not come to destroy mens lives but to save them……………………………….)Iwapo wewe ni wa Mungu wema wa Mungu lazima ukufunuke sio roho ya  ubinafsi,kiburi,ukorofi,uovu,uharibifu hukatisha tamaa na kupinga ya Mungu na kazi zake.Huwezi ukawa unasikiliza maneno ya udadisi wa uchokozi na lugha za mume wako eti….mke wako hivyo ni lugha za kuzimu ukiwa wa Mungu hizo lugha zikatae mana kama unampenda mwenzio hutkuwa mtu wa hofu na kumtafiti mwenzako 1Yoh 4:18 Kama una hofu na mwezi wako wa ndoa basi hujakamilika katika upendo hivyo ujakamilika katika upendo umekuwa mtumwa .Hiyo haitoki kwa Jehova unapoungwa katika urafiki wa kweli pendo linawafunga na roho ya kuaminiana na urafiki wenye nguvu unajengwa katika uaminifu na nia muda na nguvu Methali 3:32 Maana mtu mkaidi ni chukizo kwa bwana bali ni siri yake pamoja na wanyoofu (For the perverve person is an abomination to me Lord but His secret counsel is with upright) Yakobo 4:8 Mkaribie Mungu nae atawakaribia ninyi itakasani mikono yenu ninyi wenye dhambi ,na kusafisha mioyo yenu enyi wenye nia mbili.Ukariko wako na mtu ni uamuzi na uchaguzi wako na mtu.Mungu uwe na hiari yya upendo urafiki wowote unajengwa katika upendo na ni lazima uukuze.hautokei tu kwa bahti unahitaji nia ya mtu.Ndio maana tunaona wimbo ulio boara 1 Wakiwa wazi hisia zao kila mmoja na kuaminiana rafiki humpendae unakuwa tayari akikuambia ufanye jambo flani uonyeshwe kujali na nia yako inakuwa na shauku yenye nguvu.Ukitamani urafiki wako wenye kuendelea  hivyo hutakuwa tayari kufanya yale yanayomkwanza sababu ubinafsi haupo umeshona katika upendo na uaminifu hata pale unapogundua makosa yako mana wewe sio mkamilifu bali uamninifu kuhusu makosa na hisia.Sulemani na msichana msunami na wimbo ulio bora 6:!3(Rudi rudi (msurami)ili tukutazame kwani nnataka kumtazama msurami kama kutazama ngoma ya mahaimu?)Return return mshuramit that we may look upon you.What would you be in the shuramit as it you where the dance of the two camps)Huu ni mfano wa Yesu na kanisa.Upendo wa kweli kiasi sio rahisi mwingine huingilia na kuvunja hata kama ana nafasi ya juu na fedha mapenzi ya kweli yana sehemu yake ya haki na kibali cha MUNGU haipo nafasi ya mtu mwingine katika ndoa,mtu atamwacha baba yake na mama yake ataambatana na mke wake.Hajasema na kuambatana na mume wake kama ingekuwa hivyo kibali cha ndoa za mume kwa mume  kwa sababu ikisema mtu atambatana na babayeni sawasawa na mtu mwanaume.Hivyo mume ni kielelezo,mume ni kichwa ukisikia kichea ni kiongozi,na kama amejenga urafiki wake wa karibu na Mungu ni rahisi kuongoza maana anaongozwa Kiungu na lazima aongozwe Kiungu.Mwanzo 2:16 Agizo la Mungu lilipima wito wake wakati unamtii Mungu ni rahisi kupinga adui mwanzo 6:3 Jitie kama muhuri moyoni mwako miale ya juu.Hii ndo mana walikuwa uchi wote wawili bila kuona aibu ipo furaha ya mapenzi ya kweli.Ipo furaha ya mapenzi ya kweli na mahusiano hata lugha yao ya mapenzi ni ya pekee na kupita kiasi.Ina uzuri na nguvu usemi onyesha mkazo wa upendo/Wanaopendana wanasifiana na wanapata hata nodto,na hamu ya msichana ni kumwona mpenzi wake na kusifiana ndio tabia ya Mungu unapomsifu unambarika na unajiskia kusuma nae hata kama upo mbali anapata hamu ya upendo,hii inamwandaa kijana katika uangalizi wake na anahisi usalama zaidi.laini pia roho ya wivu Fulani hivi huja akidhani kwamba kila msichana lazima akupende(lazima akupende)ndivyo anavyodhani.Wivu wa upendo ni aina ya hamu ya shauku juu ya mtu awe wako pekee.Unajua sisi ni sura ya Mungu,nae Mungu anapenda kiasi cha kutuonea wivu roho wake anatuonea shauku tunazidi kumuwaza yeye,kuota habari zake na hii ndio ilivyo kwa unayempenda na kusikia kubarikikila wakati kwa kusema vyema juu yake
            Hatari ni pale mkristo wa ukweli kwa uchanga wake akatokea kuoa asiyeamini matokeo ni kwamba kufungamana kuambatana hakupo sababu mjenzi anapojenga mfano barabara lazima kupima udongo uliopo na ule utao sindilia ili kuweka imara barabara kwa aina ya magari yanayokusudiwa kupita ni hatari na uharibifu iwapo barabra na mkandarasi ipite tani 3 na kwa ukosefuwa ufahamu ikapita tani 18 haiwezi kustahimili ho uzoto uharibifu ni lazima.Ndio biblioa inasema Yer 17:9-10 (Moyo huea mdanganyifu kuliko vitu vyote.una ugojwa wa kufisha(kuua)nani awezae kuujua?10.mimi bwana nauchunguza moyo,navijaribu viuno,hata kumpa kila mtu kiasi cha matunda ya matendo yake)
Hivyo ni wazi kuwa mkristo mchanga hana tofauti na asiye mkristo na kwa uchanga yawezekana akaingia katika 18 za adui au mila akawa ameowa asiye amini.Paulo anasema 1Kor 7:12-14 (Yampasa abarikiwe nae tu aweza kustahimili,bali asite amni akiamini kuondoka na aondoke) 1Kor 7:12-16
Tuache kuwa ving’ang’anizi na wakati hatukupita kwa mkandarasi na kutoa vipimo yeye anajaribu viuno,(We where bone to reproduce)ndani yya viuno vya amiminiye aliye sura ya Jehova na chembechembe hai za uumbaji na akikuta kiuno tofauti,uzito tofauti na kinachotokea ni uharibifu au kifo cha mmoja  ili Mungu amuunganishe na chembechembe za kiuno zinazoleta chembechembe.chembechembe zitakazo zalisha iliyo kusudi la Mungu,ndio maana nilisema awali kwamba mkiongozwa kiungu na Mungu mtaongozwa kiungu na Mungu mdio maana Mungu alisema kwa adamu zaeni mkaongezeke mkaijaze nchi.Siku zote kile kinachofanya Mungu afurahi atabasamu kukiongeza kwa sababu katuumba kwa furaha yake ni kama vile anawwambia adamu na hawa”Nimewapenda ninasikia kutabasamu kila niwatazamapo ninyi sasa ni sura na mfano wangu hasa hivyo nataka wengine kama ninyi.”(Zaeni mkaongezeke).Ukiongozwa na Yehova kuongeka kila wakati ni lazima lakini mkiongozwa na mila na tamaa zako tu Mungu akijaribu mioyo na kupima viuno akijua mbegu ijayo itajaza uharibifu tu anawapunguza.Ndo mana Paulo anasema king’ang’anizi kwa asiye amini kama ameamua kupiga lapa mwache sababu baraka za Jehova ni kwa nyumba kwa wale wamchao ndio wataona  furaha ya kweli Zaburi 128:2 ‘Heri baraka kwa kila amchae Bwana,aendae katika njia zake.Elewa huwezi kwenda katika njia yake usipoongozwa nae na pindi akikuongoza uongezeka ni usemi wake yeye asiye sema uongo Ebr 6:18 ‘Ipo faraja kwa hao wamchao wataona upendeleo wa Jehova’ zaburi 128:3  Ndio lile tendo la alama ya kinabii wakati wameshikamana mikono na wa kushonanisha vidole,alama ya uzao kitovu cha mama hushikana na kitovu cha mtoto tumboni.’Inadhihirika nao watoto wanarithi baraka “blessing will produce blessing”na hapo inatimia ile iliyosemwa katika methali 18:22 “Apataye mke apata kitu chema”(Who he finds a wife.fings a good thing and obtains favor from the Lord)kinyume chake ni hatari ukiowa asiye amini hilo ni balaa laweza kuleta maafa,Mungu atusaidie.
Wajibu wa kuitwa au mke sio mavazi ni wajibu ujue wajibu wa mume kumpenda mkewe.Kumpenda sio maneno ni vitendo hivyo mume anapaswa kumpenda kama Kristo anavyolipenda kanisa.Yesu alijahatarisha akajitoa kwa ajili ya mkewe(kanisa)kama umeungwa na Jehova upendo ana nguvu kama mauti Ef 5:”Na unachokipenda unastaha nacho na heshima nacho ukiona hawaheshimiani fahamu ipo roho nyingine 1petr 3:7 (Husband likewise dwel with them with understanding,giving honoer to wife.as to the weaker vessel and as being theirs together of the grace of life that your prayers may not be kindered.Maombi yaweza zuiwa na kumbe sio shetani lakini u meingia katika bendi ya wajinga yya kutokumuheshimu mwenzako,nawe ukabaki unakemea shetani bila mafanikio.Mungu awahurumie wanaume shika wajibu wako kama kiongozi wa familia tunza familia usiwe mume wa kuvaa suruali bali uwe mume wajibu.1Tim 5:8 Lakini mtu yeyote asiyewafunza walio wake yaani wale wa nyumbani mwake hasa amekana imani,tena na mbaya kuliko ya mtu asiyeamini roho ya kipagani ndo inatenda kazi leo ndani yya nyumba ya MunguWako watu hujipendekeza sana kusaidia watu nje ya familia zao ndani ya familia kuna vilio nje au sifa za mtu mwema wakati ndani hajawahi kumnunulia mke chupi,sidilia n.k.Mungu atuhurumie ndipo hapo mkandarasi atapewa nafasi.Alichokiunganisha Mungu……….kama hakijaunganishwa na Mungu vilio tupu mana hakuna mwingine wa kumpa mke haki yake 1Kor 7:3,Ef 5:31 Ajabu waume wengi hutumia miili yao kama silaha hivi kila unaporudi umechoka kwa kazi umegeuka upande wa wakati mwingine kama mtumishi,umeamua kufunga na huna mpango na atendo la ndoa unaishi na mkeo kiroho roho,hapo ni mlango mpana wa adui.Lazima ujue mwili wako sio mwili wake tu ni wako na wa mkeo,ukitaka kingine katika maombi ya kujitenga mkubaliane vinginevyo bado haujafaa kutoka kwa ubinafsi,pia unapofanyam kitu jifunze kusema asante Ef 5:28-29 na mwanzo 2:22,1kor 11:3 But I want you to know that the head of every man is Christ,the head of woman is man and the head of Christ id God
Ina nafasi yako na wajibu wako na kuheshimiana usimkemee mkeo mbele ya watoto au mbele za watu hiyo ni roho ya mila za kiafrika.Lakini pia inatokana na hali ya kumuita mumeo japo ni jina la heshima  adui ameweka picha ya mzazi wako na unajua mtoto hakui kwa mzazi ndio maaana aweza kukemewa popote.Hebu jua hiyo ni rafiki mpenzi mkeo sio mama maana huwezi toa na mama yako na ikiwa umeona ni jina la heshima elewa kwamba kila jina lina mafuta yake,upako wa jina unaweza leta balaa au baraka elewa ni aina gain unamwita mwezi wako ili ufute jina la roho ifaayo kubarikiwa kwa hiyo mume inampasa kumuongoza mkewe ni ubavu ulioletwa kwako na Bwana Tuache kuokota wenyewe kwa tamaa twaweza vuta oversize,mume ni wajibu wake kumsifu mkewe usiache asifiwe na watu wengine kumbuka mshulami na Sulemani pia angalia mithali 31:28-29 wanwe huondoka na kumwita heri ,mumewe nae humsifu na kusema binti za watu wengi waamefanya mema lakini wewe umewapita wote.Hizi sifa za ndani zinainua upendo nao unapendezwa na unajua kupendwa na kupenda kunajenga afya njema ya mtu lakini Mtu anayeaibishwa lazima afya yake itamomonyoka hata kama angekula vizuri ipo nguvu ya ujenzi katika maneno mazuri mithali 5:18 ,na Mhu 9:9 chemichemi yako ibarikiwe nawe humfurahie mkeo ujana wako,zungumza na mkeo kwa upole na sio ubabe mara nyingi wanaume wasiojiamini hutumia ubabe katika maenoe yote wakidhani kuwa ndio mke atamheshimu huo ni ubagani wimbo uliobora 2:10-14 na hosea 2:14 My beloved spoke and said to me rise up my love my fair one and come away for the winter is past,the rain is over and gone,the flowers appear on the earth ,the time of singing has come ,and the voice of the turtledove is heardin our land,the jig free puts forth her green figs and th vires with the tender grapes give a good smell,Rise up my love my fair one and come away.14 oh my dove in the effects of the rock in the secter place of the cliff let me see your face,face is lovely.Yapo maneno yatulizayo moyo sio kuvunja moyo.Niliimba wimbo usemao nione nyayo zako kuna kifungu kisemacho usinisikie ee sauti ya upole na itulizayo moyo uliotaabikaa(Moyo ukitaabika unafungua mlango wa magonjwa)kutiana moyo ni moja ujenzi wa afya njema

WAJIBU WA MKE:
              Unapaswa mke kumkubali mumeo ef 5:22-24.Kor 3:18 ukisema ninkupenda mume wangu lakini sio mtii ni kiburi huo ni usanii hata Yesu alisema ukinipenda utalishika neno langu kusika ni kuwajibika katika hicho alichokisema.Biblia inasema katika Luka 9:62 Yesu akamwambia mtu aliyetia mkono wake kulima kasha akaangaliwa nyuma hafai katika ufalme wa Mungu kwa hivyo tunawaona kutii mkono ni kushika wajibu,mume na mke ni wajibu katika ufalme wa Mungu aliyompa tena kwa furaha na upendo.Hivyo mke mumewe hupokea upendeleo wa mumewe mheshimu mumeo kumheshimu mumeo ni wajibu Ester 1:20.mithali 31:23 Heshima ya mke anajenga umarufu wa mume naye hatakosa kumpa mkewe upendeleo,utii wake kwa mumewe unajenga kibali sisi waswhili tunasema mtoto anayetii anakula mara mbili maana yake ano upendeleo kipekee atakapopata ,usitii kama mtumwa bali kama rafiki kwa upendo na kujenga kinacho urafiki Tito 2:4.5  anasema kutii ni alama ya upendo mpende mumeo na kujawa na matendo mema 1petro 3:1-6 na wakati huo huo mke ndiye mtunzaji mke na familia yake mith 31:15-27 Usilale kama dume alfajiri mke amka sio utumwa ni utunzaji wa familia mke uwe na maono 16 huangalia shamba akalima ,maendeleo ya familia yanletwa na mke tena ankuwa na mmachinga…………Mke uwe na kiasi self mind katika mambo yote mruhusu Roho ili ujitawale uwe safi mchapa kazi na uwe mwema kwa watu wote hasa wale wa nyumbani mwako uwe na adabu hata unapoongea usiongee kama bata anayeharishwa hata sauti yako iwe na mvuto 1Petro 3:3-4 mpendeze mumewe 1Kor 7:34 ili uwe msaidizi wa mumeo na iwe mkaribishaji wageni Tim 5:10 hapo upendo wenu utaonyesha nguvu hautatoa nafasi kwa mtu mwingine nae Mungu atawabarikieni na kuwaongeza hata watoto wataiga maisha yenu barikiwa na Yohana Kangajaka.
*Mbele nitakuonyesha vile ambavyo adui alitaka kuniua kabisa sababu nilikuwa siamini kabisa maneno ya unabii hasa wakti wa kuoa kwangu.Nimelipa gharama na kwa rehema na neema ya Mungu amenisaidia.Nami nimelijua kosa langu,heri Mungu akujalie kujua kosa lako upate kutubu mkono wake utaku utakunua tena utakuimarisha

HUDUMA MBALIMBALI ZA MCHUNGAJI KANGAJAKA













PICHA ZA MATUKIO YA SEMINA YA NDOA







TUKIO LA SEMINA WAKATI MTUMISHI AKITOA MFANO WA JAMBO LA UPENDO
WA NDOA