Jumanne, 16 Julai 2013
SOMO EFESO 2:1-10
Neema
ya Mungu iokoayo
Utangulizi;Moyo
umeguswa kutazama japo kwa kifupi sana neno hili neema na wokovu.Faida zake na
umuhimu wake.Hebu tutazame mambo mawili haya "common grace and
saving grace"
Ufafanuzi
Katika maneno haya tunaona kana kwamba
kuna neema mbili,lakini ipo neema moja ambayo huleta utendaji kwa mpokeaji wa
makundi haya,neno hili common ni kitu cha kawaida,hivyo ipo hali ya mtu kuona
neema ya Mungu kwa kawaida sana pasipo kuruhusu kutenda kazi ndani yake na bado
Mungu akamvumilia huyo mtu akaonyesha wema wake ili apate neema ya toba.Neema hii
wenye haki na wasio haki wanaweza
kuifaidi Common grace KATIKA MWANZO 2:16-17 (Alisema kwa Adamu unayoruksa
ya kula katika kila mti wa bustani isipokuwa mti wa ujuzi wa mema na mabaya
usile,kwa maana siku utakayokula matunda ya mti huo,utakufa hakika);You may eat
the fruits of any tree in the garden
except the tree that gives knowledge of what is good and what is bad you
must not eat fruits of that tree if you do you will die the same day)
Adamu na eva walipoasi waliingizwa katika
hukumu na kutengwa na Mungu,raha ya kuwa paamoja na Mungu ikaondoka,hapo ikawa
mwanzo wa kifo na ugojwa japokuwa
wametengwa na furaha ya Mungu,wametengwa na ushirika wa Mungu,hawakufa palepale
kwa mtazamo wa nje,kwa ndani tayari sentensi ya kifo ilianza kazi yake palepale,ikaondoa amani ,ikaondoa furaha na raha ikaingiza giza la hofu
na mashaka,tabu na mateso na hapo ikawa mwanzo wa shida za mwanadamu,hapo ndipo
mtazamo wa neema hii(common grace)ukatenda kazi,neema na ufunuo wake ulikuwepo ndio mana
Adamu na Eva waliilima ardhi iliyokwisha pata laana nayo ardhi iliwapa chakula,Adamu na Eva walijenga na kufanya mambo mengi tu,kwa sababu ya neema iliyokuwa
inatangaza wema wa Mungu na uvumilivu wake.Ilikuwepo Rum 2:4 Wema wa Mungu upo
kwa watu wote kwa wema na wabaya hata leo Rum 6:23
Lakini mtu muasi Wa agizo la Jehova
hana amani,wala furaha ya kweli,hata akijitahidi kwa njia nyingi kama Adamu
na Eva,bado ni mahangaiko tu,bado ana hofu ya hukumu ya haki ya Mungu Mw 3:17-19,ipo michongoma sawasawa
na alama ya laana katika yote uyafanyayo.Taifa lolote lililoasi agizo la Mungu,hata kama yapo mengi wafanyao lakini michongoma ipo tu wanafanya kwa kuwa ipo
common grace nayo inavuta kwa uvumilivu waingie katika toba ya kweli, haipo njia
ya kuwaponya na hukumu ya haki ya Mungu,sikia kwa makini mwenye kupuunza
agizo la Mungu kwa kutumia cheo chako au dini yako au uwezo wako wa
kiuchumi.Mungu hana kivuli cha kugeukageuka katika kile alichokiagiza,vinginevyo ipo hukumu ya haki ya Mungu,ipo michongoma katika biahara zako
kitaifa na mtu mmojammoja,ipo michongama kiafya,kitaifa na mtu binafsi,lakini
sikia lipo agizo la neema iokoayo,yaani Saving grace Tito 2:11 (The grace of God
that bring salvation,that means the grace of God that save us and produce
within us godness and new spiritual life)kama alivyosema katika 2Kor 5:7 (Hata imekuwa mtu akiwa ndani ya Kristo Yesuamekuwa kiumbe kipya ya kale yamepita tazama yamekuwa mapya)Neema
ya Mungu imefunuliwa tayari katika Yesu Kristo(God grace has been revealed in Jesus Christ)Yesu alipokuja duniani neema
imekuja kwa kila mume na mke aaminiye”Through faith in Him will receive salvation.na tunapokea pia uzima wa milele .Ufu
huondolewa na Yesu aliye kifo wa kifo na ndiye aliyeishinda mauti,ndipo hapa tunaona maneno
haya mawili neema na wokovu,sababu neema,japo ipo,wokovu tunaweza tukaukosa,maana hutaki kupokea kwa imani,wadhani katika yale utendayo utaokoka,sikia ni katika
kuambatanishwa na kile Mungu alichotoa,ukikipokea kwa imani kinarejesha tena ushiririka wako na Mungu.
Wengi
wanajitahidi kutenda na kutenda chini ya laana bado ipo michongoma,pokea
kile kilichotolewa na Mungu,ndio maana wokovu wa Mungu si kazi ya dhehebu
lolote au utendaji wetu wa yale tuyafanyayo,wala sio mtindo wa utakatifu fulani,haya
yote yatakuja kama matokeo ya kupokea kile kilichotolewea na Mungu,ni toleo la
Mungu tu lifanyalo wokovu na kuingiza tabia za Mungu kama effect ya
kuambatanishwa kwako na toleo hilo la MUNGU.Maana neno wokovu ni hali ya kutoa kitu au
kuondoa katika eneo hatarishi na kukihamisha na kukiweka katika hali salama na
hali ya usalama Ebr 3:1 (Jesus is man’s representative before God as a high
priest.He was sent forth to reveal God to
men as a high priest and as an apostle as a priest.He has reconciled men to God)
Yesu
ndiye mtume na kuhani wa maungamo yetu yaani kile unachokiri kwa imani ukapokea wokovu ndicho Yesu anachokukuhania,ni Mtume na kuhani wa maungamo yetu,iwapo
unadhani waweza kuokoka kwa matendo yako,hayo sio maagizo yake Mungu.Yesu
hawezi kuwa kuhani wako,fahamu there is no other way Lawi 10:1-2 hatari iliyowakuta watendao kinyume mambo ya
Mungu na agizo lake ni mauti,Lawi 16:2 hatuingii kienyeji katika uwepo wa
Jehova,upo uharibifu, bali Mungu ameandaa njia,Yesu ndio njia ya kutuingiza nasi
tutabaki salama salimini ndani yake Hesabu 12:7 Musa anatajwa kuwa mwaminifu na
anafananishwa na YESU akiwaongoza toka misri kuelekea nchi mpya,Yesu ni mpatanishi
kwa rehema za Mungu na neema yake iokoayo ndani ya Yesu Kristo
Yesu
ni Bwana wa neema Yn 1:17 Neema na kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu,neno hili
neema ni nguvu ya kuwezesha 2Hes 2:16-17,Bwana Yesu ndiye Bwana wa amani ndani
yake Amani iliyopotezwa kwa anguko hurujeshwa tena,kwa njia zote sasa anakuwa
pamoja nasi kwa imani tunaambatanishwa tena
Pia
neema ni upendeleo wa MUNGU ambao sisi hatukustahili ingawa tulikuwa wakosaji
waasi tusiostahili,tunastahili hukumu ya haki ya Mungu,kwa upendo wake
akatusamehe bure tu,kwa neema hiyo tumekubalika katika familia ya Mungu tena,hivyo tunaona tabia hizi mbili za neema kuwa ni upendeleo wa Mungu Ef 2:8-9 upendeleo wa Mungu tusiostahili,inaonyesha pia kwamba
tunapewa msamaha na kurejeshwa katika mahusiano hata kama tulikuwa hatustahili, pia nguvu ya kuwezesha,kwa vile ni kwa nguvu zake tunaweza kubadilika 2Kor
5:17 kanuni hii ya neema inaendelea katika kutembea kwetu na Mungu katika
maeneo yetu ya imani,ni neema ya Mungu inayotusababisha kukua na kuwa na nguvu
ya Mungu na upako katika wito anaotupatia mmojammoja sio ujanja wetu 2Petro
3:18 sasa tukue tusibaki watoto tukue ili Mungu atutumie katika mchakato wa
neema,katika kumjua Bwana,hii haitegemei umri wa wokovu ulionao yawezekana bado
umebanwa katika mila na ubinafsi,neema ifanyayo kazi ni ile tu ya uvumilivu wa
Mungu,ifike mahali ambapo Mungu atakufurahia sio kukuvumilia tu,tukue katika
maarifa ya mapenzi ya Mungu,tuache utoto wa kidini na ushabiki wa kidhehebu,Baraka
za Jehova zitatujia kitaifa namtu mmojammoja,na kuruhusu shape ya Yesu sio kidhehebu
Barikiwa,
Yohana Kangajaka
Yohana Kangajaka
Imechapishwa na
Baraka Msele
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)