Alhamisi, 16 Oktoba 2014

TOKA KATIKA UHURU WA BENDERA  Yoh 10:10
Lipo hitaji la ufahamu katika kanisa la leo haswa kuhusiana na laana na ukombozi Mungu kamwe hambariki mjinga. Bali wenye ufahamu (intelligence and true knowledge ) katika kile Mungu asemacho
Wengi wanaishi katika kushindwa  na wanashangaa ziko wapi ahadi za ushindi kwa wana wa Mungu.Biblia inatuambia sisi ni vichwa sio mikia inatujulisha kuwa sisi ni zaidi ya washindi  Je Twaweza ishi katika level hiyo?
Tunahitaji mkombozi maana zipo nguvu katika ulimwengu war oho zinazo haribu Baraka zote , Afya zetu mafanikio yetu . I wapo hutakombolewa  nazo zitakupindisha hadi ushindwe kuona ahadi zake.
Tunahitaji kuona ukombozi katika mali zetu , watoto wetu, kazi zetu , biashara zetu. Tunataka ona mbadiliko pia tunataka kuyafurahia Maisha kuburudishwa katika ndoa zetu na tusitamani kufa mapema hadi umwambie yesu upesi (life is so sweet) usiwe miongoni mwa hao wanaotka wakaburudishwe Mbinguni hata hapa Mungu anataka atuburudishe.
Uzima tele vipi leo katika biashara mkia darasani mkia katika ofisi mkia sio mpango wa Jehova. Jesus came that we may have life and that we may have it more abundantly.Jicho la ufahamu likomboe maisha yako. Laana ni lugha ya dhambi au makosa tuliofanya au yaliofanywa na wakale. Ndio inaitwa Laana yale matokeo ambayo yanafanya kazi kuharibu hatima yako .Huharibu na kuzuia yale unayopaswa kuyapata wakati mwingine ni yakushindwa kutii yale Mungu alichosema . Kumb 28:15-16 (lakini itakuwa usipotaka kuisikiza sauti ya Bwana , Mungu wako, usiangalie kufanya maagizo yake yote na amri zake,nikuaagizazo hivi leo, ndipo zitakapokujua laana hizi zote na kukupata .uta laaniwa mjini, utalaaniwa  na Mashambani.
Hata uhame mji au kazi au biashara viko vizuizi vya mafanikio yako vitakufuata .Lazima awepo wakuvisemea sio Askari wako wala Mtume wala Nabii  wala kiongozi wa Dini Mungu mwenyewe mjue ili  uwe huru    yoh 8:32  (Tena mtaifahamu kweli, na hiyo kweli itawaweka huru.) 1kor 6:16-18 (Au hamjui yakuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili umoja naye? Maana asema ,wale wawili watakao kuwa mwili mmoja. Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho naye .ikimbieni zinaa .Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwli wake;ila yeye afanyaye zinzaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe .)Kumbuka hata kuzungumza neno la kweli safi toka kwa Mungu nihadi uwe umekombolewa na hofu za watu.( We can speak apure word from God unit we are delivered  from the fear of man and desire for man’s recognition and acceptance .) mpendwa haijalishi kukubaliwa na watu  kombolewa na hofu za watu uwe na hofu ya Mungu kombolewa toka kikabila cha watu. Tusitazame mambo kwa interest za watu huo ni mtego (it will be stumbling block.


Mtumshi wa MUNGU Nasari Elietha wakipeana mkono na Mtumishi Yohana Kangajaka katika semina ya neno la MUNGU ulilofanyika katika kanisa la KKKT Mkanjuni Tanga


Haleluya tunamshukuru mungu kwa kutupa siku nyingine ambayo tumeona nguvu zake zikitenda kazi kupitia mchungaji Yohana Kangajaka sasa tupo tanga katika semina ya neno la MUNGU kwenye Usharika wa mikanjuni kanisa la KKKT