Jumapili, 15 Desemba 2013

Aliyemtangulia Bwana



Learn The Holy bible with Ev Yohana Kangajaka (Jifunze Biblia na Ev Yohana Kangajaka)

ALIYEMTANGULIA BWANA


Neno Bwana likiandikwa kwa herufi BWANA linamzungumza Mungu,Adonai au yahwe ambayo badae walitamka Yehova.Yehova maana yake ni Mungu muumbaji,yeye aishie kwa uwezo wake mwenyewe,Adonai Bwana mkubwa,akitaka kwenda mahali wakao marafiki zake anawajulisha wao ndio wanaojua njia atakayopitia ,wanaanda mazingira kuwaweka watu tayari,kumngojea na hivyo kuna watu wanatangulia,na ving’ora ili kusafisha njia Bwana mkubwa asiweke foleni,Ving’ora hivyo ndio sauti ya kinabii,na mmoja aliyeitwa sauti ya mtu aliyae nyikani ambaye alimtangulia Bwana kusafisha njia,jina lake aliitwa Yohana

Mungu akitaka kufanya jambao lolote kwa mtu,kwa taifa au kwa dunia lazima awajulishe hiyo siri marafii zake ambao ni manabii,Nabii ni king’ora cha mbinguni,ni sauti ya mgutusho, Amosi 3:7 (Hakika Bwana Mungu hatafanya neno lolote,bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake.) Kwa hiyo Yohana alikuwa rafiki wa Mungu maana nabii ni rafiki wa Mungu,ni mkalimani wa kile Mungu asimacho,kuwaanda watu waweze kuruhusu uwepo wake.Yohana aliwaagiza watu wote watubu bila kujali walikuwa watu gani,wa cheo gani,wa dini gani maadamu ni mtu alipaswa kutubu,kwa sababu Mungu hana upendeleo,njia yake anayopitia akitaka kufanya kitu ni mioyo ya watu wenye toba,hebu jifunze kuheshimu sauti za kinabiii badala ya kupambana ingia katika Toba ili Bwana akuandae kumruhusu Bwana mkubwa Isaya 57:15 (Maana yeye aliyejuu,aliyetukuka,akaaye milele;ambaye jina lake ni mtakatifu asema hivi,nakaa mimi mahali palipo inuka,palipo patakatifu,tena pamoja na yeye aliye na roho iliyotubu na kunyenyekea,ili kuzifufua roho za wanyenyekevu,na kufufua mioyo yao waliotubu.)


Hebu jinyenyekeshe na uwe na toba ya kwelikweli,ghahiri njia zako mbaya uache uovu wako ili uwe chombo cha kubeba kusudi la Mungu Mt 3:7 -10 (Hata alipoona wengi miongoni mwa mafarisayo na masudukayo wakiujiaa ubatizo wake,aliwaambia,Enyi uzao wa nyoka,ni nani aliwaonya ninyi kuikimbia hasira itakayokuja?,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,)Wakati Mungu alipotaka kuibadilisha historia ya mwanadamu,alimtuma mjumbe maalumu katika injili ya luka 1:26 (Mwezi wa sita malaika Gabrieli alitumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa Galilaya jina lake Nazaret) Ukiona neno malaika maana yake ni mjumbe maalumu 

Endelea kufuatilia pia mafundisho mbalimbali kupia Youtube @http://www.youtube.com/my_videos?o=U

Also via Our page on Facebook

Follows us on Facebook

@https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1434806840071091&set=a.1426829134202195.1073741828.100006253653384&type=1&theater&notif_t=photo_comment..

Yohana Kangajaka

Somo la Leo ni kutoka katika Injili ya Yohana 1:12 (Bali waliompokea aliwapa uwezo kufanyika watoto wa Mungu,ndio wale waliaminio jina lake;)

Mchungaji Kiongozi akifungua Mkutano pamoja na Mkuu wa Dinari unaoanza Leo na kuisha Siku ya Jumapili ijayo

 Neno la Ufunguzi wa Mkutano linatoka Luka 1:26 (Mwezi wa sita,Malaika Gabrieli alitumwa kwenda mpaka Mji wa galilaya jina lake nazareth.,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,)  

 Mchungaji  Kiongozi Leus Shemkala wa Kanisa la KKKT Usharika wa Handeni,akikaribisha makutano pamoja na wageni mbalimbali waliohudhuria Mkutano.Jina la Bwana libarikiwe




Yohana Kangajaka
Somo la Leo ni kutoka katika Injili ya Yohana 1:12 (Bali waliompokea aliwapa uwezo kufanyika watoto wa Mungu,ndio wale waliaminio jina lake;)