Spiritual voice ni huduma ambayo ilianza miaka 32 iliyopita 1982,ni maono ambayo Ev Yohana Kangajaka aliyapata miaka miwili tu baada ya kuokoka.Mungu alimwonyesha akiwafikia waliopotea katika maeneo mbalimbali,alipopata maono hayo aliingia kwenye maombi ya kufunga kwa siku arobaini(40),nae akaanza kufuatlia maeneo ambayo hayajafikiwa na Injili akijitolea kwa Gharama zake na pia aliyashirikisha maono haya kwamba "kama unampenda Mungu,kuufikia ulimwengu na kuwatafuta walipotea ndio maono ya Mungu"na kuwasaidia wachanga kiroho kufikia ukomavu waweze kuwa vyombo vya Mungu,kwa neema ya Mungu aliwezesha vijana kupata msukumo huo kuungana nae katika wajibu na sasa ni Watumishi wakubwa na wanmtumikia Mungu ipasavyo.Ijapokuwa amekutana na upinzani mwingi kwa viongozi wa kidini wakidhani kwamba anaanzisha dini nyingine lakini lengo lake ni kuwafanya watu wajue maono ya Mungu yohana 3:16 "Kama Mungu alimtoa mwanae wa pekee kwa ajili ya ulimwengu msukumo huo lazima uwepo ndani ya watu wa Mungu kijitoa kwa ajili ya ulimwengu vinginevyo watenda dhambi watafia dhambini na wachanga kiroho watabaki wachanga milele kama hatutapokea mzigo huo"
Katika nchi ya Tanzania amezunguka karibuni mikoa yote Bara na Visiwani na Afrika mashariki pamoja na Afrika ya kati na nchi za Ulaya
Na huku kote ameona kiu ya watu katika kumtafuta Mungu na nguvu za Mungu zikionekana akiwafungua watu
Kwa sasa anafanya Huduma na makanisa ya KKKT Kama mmisionari japo hufanya Huduma popote anapoalikwa katika madhehebu yote pale wanapomhitaji
BARIKIWA NA BWANA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni