Kila mwanadamu hufuarahia sana anapofanya jambo lolote na watu wakalikubali ndani yake hujiskia vizuri na wanadamu wana mambo wanayoangalia kumkubali mtu,utazama ukoo anaotoka,familia uliozaliwa.Hutazama kiwango chako cha elimu na kiwango chako cha kiuchumi,hivyo wanakutazama muonekano wako kuanzia kichwani hata miguuni wanasema "huyu ni njema mwanangu",Hivyo huo ni mtazamo wa mwanadamu anavyomtazama mtu bali Mungu anamtazama tofauti Mungu anatazama sura ya ndani sio muonekano wa nje ambao unawakilisha uweza wako wa kiuchumi,kielemu,kiukoo,kicheo watu wanaweza kukupongeza wakasema huyu ni njema sana lakini kesho wakakusulubisha haohao waliokupongeza ndio haohao wanakusulubu tena hawa ni wanadamu tu usitafute kibali cha wanadamu tafuta kibali cha Mungu,heri yako ukakubaliwa na Jehova kuliko wanadamu.Katika somo hili tunamwona Yesu na wanafunzi wake wakiingia katika wilaya ya Gerasi ambayo iko kusini mashariki mwa ziwa galilaya,wenyeji wake wengi walikuwa wapagani ndio walioitwa wagerasi.Yesu alikutana na mtu huko aliyeishi makaburini na unajua makaburi sio mahali pa furaha wala sio mahali pa kufanyia piknic ni mahali pa hofu,mahali pa mashaka.mahali pa wasiwasi,mahali pa huzuni,unatambua mtu yule aliishi kwa namna hiyo,maisha ya mashaka,maisha ya huzuni,kama vile leo wengi wetu wanaonekana wanishi mijni kwenye majumba makubwa kumbe mioyo yao imejaa mashaka,imejaa huzuni,imejaa wasiwasi hawana amani na ndugu zao,hawana furaha hata na familia zao hawafurahii hata kazi zao,wana mashaka katika vyeo vyao wako makaburini kw amtazamo wa nje waweza kuwasifu kana kwamba wako njema kumbee Yesu akiwatazama wako katika wilaya ya Gerasi na wanajeshi wamebeba jeshi la matatizo na huzuni Yesu anawahurumia.anaamua leo kujihatarisha na kupita katika maeneo yalio najisi,makaburi yako ni yapi?Jambo gani limeiba furaha yako,afya yako,amani yako umeipotezea wapi japokuwa hata ulionao ofisini hawajui hata mume wako au mke wako hajui kwamba upo makaburini wanabaki kukusifia kwamba upo njema kumbe umebakia kuzikwa tu Yesu anatambua ulivyo anapita katika njia yako bila kujali Yeye ni Mtakatifu asingepita ,mahali pachafu lakini ametambua kwamba makaburini kuna mtu ambaye ni sura ya Mungu ni mfano waMungu anataka kukukomboa kutoka katika mikono ya jeshi la uovu mana anaijua shida yako,anaona sura ya ndani amekukubali ulivyo Mtu huyu wa wagerasi watu walimuona mwendawazimu kama vile ambavyo wachache walijua shida yako hata wewe japo hawajui yote wamekupa jina wengine wamekuita ombaomba na wengine wamekuita mkopaji ukitokea tu wengine wanondoka wanajua hayo ni majina ya watu yasikukatishe tamaa Yesu amekukubali anaona sura yake na mfano wake anakuja akukomboe,Mtu huyu aliyekuwa anapepo wachafu alimwona Yesu kwa mbali alimtambua kuwa ni Mwana wa Mungu alielewa kuwa atakuja kuwahukuwa siku moja alikasiriswa na ujio ule mana alijua majira ya hukumu yao bado.Pepo walikasirika wakamwambia Yesu mbona unakuja kutusumbua kabla ya wakati "Tuna nini nawe Yesu mwana wa Mungu"Ajabu ni kwamba mapepo wanatambua kuwa Yesu ni mwana wa Mungu ni fedheha na Aibu kwamba kuna watu wamezidiwa akili na Mapepo hawajui kwamba Yesu ni mwana wa Mungu,wanakana UMUNGU wa Yesu sikia mwana wa nyoka ni nyoka.Mwana wa Mungu ni Mungu tumia akili sawasawa.Yesu aliona thamani ya mtu huyu kuliko mali aliona lazima mapepo yamwachie mana yeye ni sura ya Mungu asingetaka sura yake iharibiwe na roho chafu za ulevi,za ufisadi na udhalimu wote amepita njia yako acha kukasirika ukiona amegusa maisha yako acha kuokota mawe ya kumpigia Yesu na kupiga teke huruma zake na upendo wake kukufuatilia sababu wewe si wa shetani mana shetani hajakuumba ameiba tu heshima yako amekuvua nguo kama yule mgerasi anauchungu na wewe weka mawe yako chini acha maneno ya ubishi.Yesu amekukubali ulivyo yalokufunga lazima yakuachilie.Thamani yako ni kubwa yuko tayari Yesu mapepo yaingie kwa nguruwe wewe uwe huru.Leo ukimpa uchaguzi shetani kati ya mali na mtu yeye atachagua mtu hata kama eneo limejaa dhahabu na gesi kama kule Mtwara.Sikia ndugu yangu thamani yako ni kubwa kuliko tamaa yako ya mali na ufisadi acha kutoa muhanga maisha yako kwa ajili ya mali usizidiwe akili na shetani usije ukaingia katika bendi ya Jinga Jazz Bend ukauza utu wako na heshima yako kwa vitu jijue dhamani yako hata kama wengine hawakukubali kwa sababu ya itikadi zako za kidini au kichama Yesu anakukupenda amekukubali ulivyo amepitia njia yako akukomboe usipate shida kama wakikukataa Mungu akikubali atajaliza mapungufu yako yote kwa sababu Mungu ni kila kitu amini upendo wake na pokea upendo wake kwa imani jeshi lijapojipanga kupigana nawe usiogope halitakuweza ataliamuru kwa neno lake nalo litatawanyika Yeye ndiye mwenye mamlaka yote duniani na mbinguni,ana mamlaka juu ya nguvu zote za giza Yeye ni Mfalme mkuu aweaa kukuvisha na kukufunika aibu yako kama alivyomvisha huyu mgerasi atarejesha Heshima yako,afya yako atarejesha uchumi wako ulitekwa na chuma ulete,atarejesha furaha yako utakuwa ushuhuda leo ukiamini yote yawezekana kwake aaminiye,amekubali hebu jikubali mwenyewe ili furaha yako ijalizwe.AMEN