Jumamosi, 20 Julai 2013
Hubiri
SHIDA
HAINA UBAGUZI
AYUBU
5:7
Bali binadamu huzaliwa apate
taabu,kama cheche za moto zirukavyo
juu.Shida haibagui watu.Kila mmoja zipo nyakati anakutana na tatizo tena
nyakati za ambazo huwezi kudhania.Kipindi ambacho unaona mambo yote ni
swari kila kitu ni salama kisha punde
ghafka bin vupu shida
hiyoooo........!inakukumba.Mungu ajua kwamba taabu itakujia anakupangia mpango
wa kufanya ,anataka kukusaidia ili uweze kutatua bila kurukwa na akili.Je ni
nani aletaye shida?Yn 10:10 (Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu,mimi
nalikuja ili wawe na uzima,kisha wawe nao tele),2Tim 2:9
Sio
shida zote zianzishwanzo na ibilisi ,nyingine wewe mwenyewe waweza anzisha unapokiuka neno la Mungu 2Thel 2:2(Kwamba msifadhaiswe haraka
hata kuiacha nia yenu ,wala msitishwe kwa roho,wala kwa neno,wala kwa waraka
unaodhaniwa kwamba ni wetu,kana kwamba siku ya Bwana ilikwisha kuwapo)maneno
yaweza anzisha shida na kinywa hunena yaliyoujaza moyo.Tumeshidwa kujaza neno
la Mungu na hii ni chanzo cha shida Tanzania.Acheni kunena habari mbaya tu,japo
kila mmoja atakumbwa na huzuni bali walijuao neno ni washindi,wakati wa shida
utajua hata rafiki wa ukweli na wale wa uongo.Yesu ndiye rafiki wa kweli.
Matatizo
na shida vyaweza kufanya mtu awe mkali kwa kila mmoja Lk10:41 Martha alimjia
Yesu akiwa na hasira kwa hiyo mariamu hakupenda kumsaidia,Yesu alimjibu shida
huzidisha hasira,hatari zaidi waweza patwa na ugojwa kwa ajili ya hasira Zab
102:3-5 Unapopatwa na shida unakosa usingizi,unakosa hamu ya kula,afya yako
yadhohofika.Ndg hakuna aliye mshindi wakati huu wa shida lakini tunatiwa moyo
kujua kwamba Mungu ametupa njia ya Ushindi kwa hiyo ibilisi akija na shida
anamkuta Yesu akiwa pamoja nasi tena hata kama ulijeletea mwenyewe na kila
mmoja anajua anavuna ulichokipanda bado Yesu hakulaumu anataka kukusaidia Mith
25:19.Usitegemee mwanadamu wakati wa taabu,mtu si mwaminifu,Mungu ni mwaminifu.
Hata
wakija watu wewe mtazame Mungu zaidi sio watu ama sivyo utajikwanza bure Zab
50:15(Niite wakati wa taabu……)Tanzania hiki sio kipindi cha kuteta na kubaguana
.Tuinuke na tumlilie Mungu tusirukiane na kuonyeshana vidole tujikubali na
tuinue mikono kwa Jehova Yn 14:1 (Hapo
mwanzo palikuwako na Neno naye Neno alikuwako
kwa Mungu,naye Neno alikuwa Mungu)
Shida
inapokupata cheche zake zinapokuchoma usiache moyo wake ufadhaike Yn 14:8.Beba
amani ya Yesu katika taabu,ndio zawadi
pekee ipitayo fahamu zote ipokee leo Yesu ndie mfalme wa amani 2Kor 4:8 (Pande zote twadhikika bali hatusongwi,twaona
shaka bali hatukati tamaa)Hatuachwi hii
ni ahadi yake yeye aliye wa kweli na mwaminifu 2Nyakati 32:17 Hezekia baba yake alikuwa mwovu sana
aliitwa Ahazi alisababisha Taifa nzima
la Israeli waabudu sanamu lakini Hezekia hakufuata njia za baba yake wala
hakumlaumu baba yake,kwamba ameshababisha shida ndani ya Taifa.Ukitaka msaada wa Mungu usijaribu kumlaumu mwingine
itakuingiza kwenye uchungu tu na kualika
uharibifu,lawama haijengi,inabomoa simama kwa toba mbele za Jehova
ukilitenda neno la Mungu Mambo ya nyakati
32:2-7 Hezekia alijiandaa kushinda katikati ya hali ya kutisha,hakukata
tamaa maana kukata tamaa ni kiti cha shetani,ujasiri wa Hezekia hauko kwa watu
bali kwa Bwana,ukiwa na ujasiri kwa Mungu wewe ni mshindi kabla ya mashindano,ukiwa
katika taabu chunga sana kinywa chako usije ukafanana na Martha na kulalamikia
wengine manung’uniko yanaleta shida,Martha alikemewa na Bwana,uwe imara na
hodari usiogope wala usifadhaike mbele za mfalme wa Ashuru.Tuliyenaye ni mkuu
kuliko aliye na mfalme senakarebu,haijalishi moyo wako umekumbwa na majaribu
gani,haijalishi nchi yako imekumbwa na
maswaibu gani Rum8:31(Basi tusime nini
juu ya hayo,Mungu akiwa upande wetu ni nani aliye juu yetu?),mpe nafasi Mungu awe upande wako uwepo wa Mungu ukiwa
pamoja na wewe wewe ni mshindi maana Mungu ni kila kitu.
Barikiwa
Yohana Kangajaka
Imechapiswa na Baraka
Msele
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)