Jumapili, 30 Juni 2013
Jumamosi, 29 Juni 2013
video
MAHUBIRI YA LEO KATIKA KANISA LA KKKT USHARIKA WA KOROGWE
KARIBU KATIKA MAHUBIRI YA LEO
REJECTED OFFERING (SADAKA ILIYOKATALIWA)
YA CAIN AND ABEL.
Ni huzuni ukiwa umejiandaa kumtolea Mungu halafu sadaka yako ikakataliwa.Ipo huzuni,aibu,na hasira hasa ukimtazama uliyenae akiwa amepata kibali na sadaka yake ikikubaliwa.Jifunze kutii na kufanya sawa na maelekezo ya Mun gu ili umfanye Mungu kukufurahia na sadaka utoayo pia.Kiebrania THUSIA maana yake ni yule mtoaji dhabihu or sacrifice victim kwa hikyo sio suala la sadaka bali Mungu huangalia na mhusika mtoaji(moyo wako ulivyo)Kaini alishidwa kumtii MUNGU akafanya alichoona kizuri kumbe ni cha udongo tu yaani cha hekima ya kibinadamu na akili ya mwili tu sio divine amangement na elekezo halionyeshi kama alifanya kwa imani Ebr 11:4 (Kwa imani habili alimtolea Mungu dhabihu iliyo bora kuliko kaini;kwa hiyo alishuhudiwa kuwa ana haki,Mungu akazishuhudia sadaka zake na kwa hiyo ijapokuwa amekufa angalia akinena.) Sadaka iliyotolewa kwa mangali na elekezo la Kimungu kwa imani ina uhai na inaongea,Biblia haionyheshi kuwa Abeli alifanya kwa imani yeye alifanya kwa mtazamo wa mwili tu.
2Kor 5:7 (Maana twaenenda kwa imani si kwa kuona)Je imani twaipataje? Rum 10:17 (Basi imani chazo chake ni kusikia na kusikia huja kwa neno la Kristo) Kusikia ni itikio la utii kwa kile kisemwacho .;kumbuka Ebra 12:24 (Na Yesu ni mjumbe wa Agano jipya na Damu yakunyuyizwa,inenayo mema kuliko ile ya Habili.
BWANA YESU APEWE SIFA NA SHUKRANI
Ijumaa, 28 Juni 2013
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)