Jumamosi, 20 Julai 2013

Hubiri



                                        SHIDA HAINA UBAGUZI
AYUBU 5:7
                   Bali binadamu huzaliwa apate taabu,kama cheche  za moto zirukavyo juu.Shida haibagui watu.Kila mmoja zipo nyakati anakutana na tatizo tena nyakati za ambazo huwezi kudhania.Kipindi ambacho unaona mambo yote ni swari   kila kitu ni salama kisha punde ghafka  bin vupu shida hiyoooo........!inakukumba.Mungu ajua kwamba taabu itakujia anakupangia mpango wa kufanya ,anataka kukusaidia ili uweze kutatua bila kurukwa na akili.Je ni nani aletaye shida?Yn 10:10 (Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu,mimi nalikuja ili wawe na uzima,kisha wawe nao tele),2Tim 2:9
Sio shida zote zianzishwanzo na ibilisi ,nyingine wewe mwenyewe  waweza anzisha unapokiuka neno  la Mungu 2Thel 2:2(Kwamba msifadhaiswe haraka hata kuiacha nia yenu ,wala msitishwe kwa roho,wala kwa neno,wala kwa waraka unaodhaniwa kwamba ni wetu,kana kwamba siku ya Bwana ilikwisha kuwapo)maneno yaweza anzisha shida na kinywa hunena yaliyoujaza moyo.Tumeshidwa kujaza neno la Mungu na hii ni chanzo cha shida Tanzania.Acheni kunena habari mbaya tu,japo kila mmoja atakumbwa na huzuni bali walijuao neno ni washindi,wakati wa shida utajua hata rafiki wa ukweli na wale wa uongo.Yesu ndiye rafiki wa kweli.
Matatizo na shida vyaweza kufanya mtu awe mkali kwa kila mmoja Lk10:41 Martha alimjia Yesu akiwa na hasira kwa hiyo mariamu hakupenda kumsaidia,Yesu alimjibu shida huzidisha hasira,hatari zaidi waweza patwa na ugojwa kwa ajili ya hasira Zab 102:3-5 Unapopatwa na shida unakosa usingizi,unakosa hamu ya kula,afya yako yadhohofika.Ndg hakuna aliye mshindi wakati huu wa shida lakini tunatiwa moyo kujua kwamba Mungu ametupa njia ya Ushindi kwa hiyo ibilisi akija na shida anamkuta Yesu akiwa pamoja nasi tena hata kama ulijeletea mwenyewe na kila mmoja anajua anavuna ulichokipanda bado Yesu hakulaumu anataka kukusaidia Mith 25:19.Usitegemee mwanadamu wakati wa taabu,mtu si mwaminifu,Mungu ni mwaminifu.
Hata wakija watu wewe mtazame Mungu zaidi sio watu ama sivyo utajikwanza bure Zab 50:15(Niite wakati wa taabu……)Tanzania hiki sio kipindi cha kuteta na kubaguana .Tuinuke na tumlilie Mungu tusirukiane na kuonyeshana vidole tujikubali na tuinue mikono kwa Jehova  Yn 14:1 (Hapo mwanzo palikuwako na Neno naye Neno alikuwako  kwa Mungu,naye Neno alikuwa Mungu)
Shida inapokupata cheche zake zinapokuchoma usiache moyo wake ufadhaike Yn 14:8.Beba amani ya Yesu  katika taabu,ndio zawadi pekee ipitayo fahamu zote ipokee leo Yesu ndie mfalme wa amani 2Kor 4:8  (Pande zote twadhikika bali hatusongwi,twaona shaka  bali hatukati tamaa)Hatuachwi hii ni ahadi yake yeye aliye wa kweli na mwaminifu 2Nyakati  32:17 Hezekia baba yake alikuwa mwovu sana aliitwa Ahazi alisababisha Taifa  nzima la Israeli waabudu sanamu lakini Hezekia hakufuata njia za baba yake wala hakumlaumu baba yake,kwamba ameshababisha shida ndani ya Taifa.Ukitaka  msaada wa Mungu usijaribu kumlaumu mwingine itakuingiza kwenye uchungu tu na kualika  uharibifu,lawama haijengi,inabomoa simama kwa toba mbele za Jehova ukilitenda neno la Mungu Mambo ya nyakati  32:2-7 Hezekia alijiandaa kushinda katikati ya hali ya kutisha,hakukata tamaa maana kukata tamaa ni kiti cha shetani,ujasiri wa Hezekia hauko kwa watu bali kwa Bwana,ukiwa na ujasiri kwa Mungu wewe ni mshindi kabla ya mashindano,ukiwa katika taabu chunga sana kinywa chako usije ukafanana na Martha na kulalamikia wengine manung’uniko yanaleta shida,Martha alikemewa na Bwana,uwe imara na hodari usiogope wala usifadhaike mbele za mfalme wa Ashuru.Tuliyenaye ni mkuu kuliko aliye na mfalme senakarebu,haijalishi moyo wako umekumbwa na majaribu gani,haijalishi nchi yako imekumbwa  na maswaibu gani  Rum8:31(Basi tusime nini juu ya hayo,Mungu akiwa upande wetu ni nani aliye juu yetu?),mpe nafasi  Mungu awe upande wako uwepo wa Mungu ukiwa pamoja na wewe wewe ni mshindi maana Mungu ni kila kitu.
                                      Barikiwa
                                                         Yohana Kangajaka
                       Imechapiswa na Baraka Msele       

Hakuna maoni: