Jumanne, 16 Julai 2013

SOMO EFESO 2:1-10



Neema ya Mungu iokoayo
Utangulizi;Moyo umeguswa kutazama japo kwa kifupi sana neno hili neema na wokovu.Faida zake na umuhimu  wake.Hebu tutazame mambo mawili haya "common grace and saving grace"
Ufafanuzi

    Katika maneno haya  tunaona kana kwamba kuna neema mbili,lakini ipo neema moja ambayo huleta utendaji kwa mpokeaji wa makundi haya,neno hili common ni kitu cha kawaida,hivyo ipo hali ya mtu kuona neema ya Mungu kwa kawaida sana pasipo kuruhusu kutenda kazi ndani yake na bado Mungu akamvumilia huyo mtu akaonyesha wema wake ili apate neema ya toba.Neema hii  wenye haki na wasio haki wanaweza kuifaidi  Common grace KATIKA MWANZO 2:16-17 (Alisema kwa Adamu unayoruksa ya kula katika kila mti wa bustani isipokuwa mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile,kwa maana siku utakayokula matunda ya mti huo,utakufa hakika);You may eat  the fruits of any tree in the garden except  the tree that gives  knowledge of what is good and what is bad you must not eat fruits of that tree if you do you will die the same day)
   Adamu na eva walipoasi waliingizwa katika hukumu na kutengwa na Mungu,raha ya kuwa paamoja na Mungu ikaondoka,hapo ikawa mwanzo wa kifo na ugojwa  japokuwa wametengwa na furaha ya Mungu,wametengwa na ushirika wa Mungu,hawakufa palepale kwa mtazamo wa nje,kwa ndani tayari sentensi ya kifo ilianza kazi yake palepale,ikaondoa amani ,ikaondoa furaha na raha ikaingiza giza la hofu na mashaka,tabu na mateso na hapo ikawa mwanzo wa shida za mwanadamu,hapo ndipo mtazamo wa neema hii(common grace)ukatenda kazi,neema na ufunuo wake ulikuwepo ndio mana Adamu na Eva waliilima ardhi iliyokwisha pata laana nayo ardhi iliwapa chakula,Adamu na Eva walijenga na kufanya mambo mengi tu,kwa sababu ya neema iliyokuwa inatangaza wema wa Mungu na uvumilivu wake.Ilikuwepo Rum 2:4 Wema wa Mungu upo kwa watu wote kwa wema na wabaya hata leo Rum 6:23
       Lakini mtu muasi Wa agizo la Jehova hana amani,wala furaha ya kweli,hata akijitahidi kwa njia nyingi kama Adamu na Eva,bado  ni mahangaiko tu,bado ana hofu ya hukumu ya haki  ya Mungu Mw 3:17-19,ipo michongoma sawasawa na alama ya laana katika yote uyafanyayo.Taifa lolote lililoasi agizo la Mungu,hata kama yapo mengi wafanyao lakini michongoma ipo tu wanafanya kwa kuwa ipo common grace nayo inavuta kwa uvumilivu waingie katika toba ya kweli, haipo njia ya kuwaponya na hukumu ya haki ya Mungu,sikia kwa makini mwenye kupuunza agizo la Mungu kwa kutumia cheo chako au dini yako au uwezo wako wa kiuchumi.Mungu hana kivuli cha kugeukageuka katika kile alichokiagiza,vinginevyo ipo hukumu ya haki ya Mungu,ipo michongoma katika biahara zako kitaifa na mtu mmojammoja,ipo michongama kiafya,kitaifa na mtu binafsi,lakini sikia lipo agizo la neema iokoayo,yaani Saving grace Tito 2:11 (The grace of God that bring salvation,that means the grace of God that save us and produce within us godness and new spiritual life)kama alivyosema katika 2Kor 5:7 (Hata imekuwa mtu akiwa ndani ya Kristo Yesuamekuwa kiumbe kipya ya kale yamepita tazama yamekuwa mapya)Neema ya Mungu imefunuliwa tayari katika Yesu Kristo(God grace has been revealed  in Jesus Christ)Yesu alipokuja duniani neema imekuja kwa kila mume na mke aaminiye”Through faith in Him will receive  salvation.na tunapokea pia uzima wa milele .Ufu huondolewa na Yesu aliye kifo wa kifo na ndiye aliyeishinda mauti,ndipo hapa tunaona maneno haya mawili neema na wokovu,sababu neema,japo ipo,wokovu tunaweza tukaukosa,maana hutaki kupokea kwa imani,wadhani katika yale utendayo utaokoka,sikia ni katika kuambatanishwa na kile Mungu alichotoa,ukikipokea kwa imani kinarejesha tena ushiririka wako na Mungu.
Wengi wanajitahidi kutenda na kutenda chini ya laana bado ipo michongoma,pokea kile kilichotolewa na Mungu,ndio maana wokovu wa Mungu si kazi ya dhehebu lolote au utendaji wetu wa yale tuyafanyayo,wala sio mtindo wa utakatifu fulani,haya yote yatakuja kama matokeo ya kupokea kile kilichotolewea na Mungu,ni toleo la Mungu tu lifanyalo wokovu na kuingiza tabia za Mungu kama effect ya kuambatanishwa kwako na toleo hilo la MUNGU.Maana neno wokovu ni hali ya kutoa kitu au kuondoa katika eneo hatarishi na kukihamisha na kukiweka katika hali salama na hali ya usalama Ebr 3:1 (Jesus is man’s representative before God as a high priest.He was sent forth to reveal  God to men as a high priest and as an apostle as a priest.He has reconciled men to God)
Yesu ndiye mtume na kuhani wa maungamo yetu yaani kile unachokiri kwa imani ukapokea  wokovu ndicho Yesu anachokukuhania,ni Mtume na kuhani wa maungamo yetu,iwapo unadhani waweza kuokoka kwa matendo yako,hayo sio maagizo yake Mungu.Yesu hawezi kuwa kuhani wako,fahamu there is no other way Lawi 10:1-2  hatari iliyowakuta watendao kinyume mambo ya Mungu na agizo lake ni mauti,Lawi 16:2 hatuingii kienyeji katika uwepo wa Jehova,upo uharibifu, bali Mungu ameandaa njia,Yesu ndio njia ya kutuingiza nasi tutabaki salama salimini ndani yake Hesabu 12:7 Musa anatajwa kuwa mwaminifu na anafananishwa na YESU akiwaongoza toka misri kuelekea nchi mpya,Yesu ni mpatanishi kwa rehema za Mungu na neema yake iokoayo ndani ya Yesu Kristo
Yesu ni Bwana wa neema Yn 1:17 Neema na kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu,neno hili neema ni nguvu ya kuwezesha 2Hes 2:16-17,Bwana Yesu ndiye Bwana wa amani ndani yake Amani iliyopotezwa kwa anguko hurujeshwa tena,kwa njia zote sasa anakuwa pamoja nasi kwa imani tunaambatanishwa tena
Pia neema ni upendeleo wa MUNGU ambao sisi hatukustahili ingawa tulikuwa wakosaji waasi tusiostahili,tunastahili hukumu ya haki ya Mungu,kwa upendo wake akatusamehe bure tu,kwa neema hiyo tumekubalika katika familia ya Mungu tena,hivyo tunaona tabia hizi mbili za neema kuwa  ni upendeleo wa Mungu Ef 2:8-9  upendeleo wa Mungu tusiostahili,inaonyesha pia kwamba tunapewa msamaha na kurejeshwa katika mahusiano hata kama tulikuwa hatustahili, pia nguvu ya kuwezesha,kwa vile ni kwa nguvu zake tunaweza kubadilika 2Kor 5:17 kanuni hii ya neema inaendelea katika kutembea kwetu na Mungu katika maeneo yetu ya imani,ni neema ya Mungu inayotusababisha kukua na kuwa na nguvu ya Mungu na upako katika wito anaotupatia mmojammoja sio ujanja wetu 2Petro 3:18 sasa tukue tusibaki watoto tukue ili Mungu atutumie katika mchakato wa neema,katika kumjua Bwana,hii haitegemei umri wa wokovu ulionao yawezekana bado umebanwa katika mila na ubinafsi,neema ifanyayo kazi ni ile tu ya uvumilivu wa Mungu,ifike mahali ambapo Mungu atakufurahia sio kukuvumilia tu,tukue katika maarifa ya mapenzi ya Mungu,tuache utoto wa kidini na ushabiki wa kidhehebu,Baraka za Jehova zitatujia kitaifa namtu mmojammoja,na kuruhusu shape ya Yesu sio kidhehebu
                          Barikiwa,
                                         Yohana Kangajaka
                                                                               Imechapishwa na Baraka Msele     

Hakuna maoni: