Ijumaa, 5 Julai 2013

SOMO

                                             NIDHAMU YA KUSIKILIZA
   The discipline of heeding Math 10:27 (Nawaambieni ninyi kkatika giza lisemeni katika nuru na msikialo kwa siri lihubirini juu ya nyumba.
Kumbe ziko nyakati ambazo Mungu anatuweka katika nidhamu katika giza na hutufundisha kumsikiliza yeye.Viko vitu vingi hutujia ili tuvisikilize lakini katika giza jifunze kutulia katika mikono ya Mungu aliye hai na kuimba sifa zake wala sio kuongea giza lako ili ubakie katika uvuli wa mikono ya Jehova hata utakapo jifunza kusikiliza na kusikiliza sauti yake isemayo katika giza anasema niwaambialo ninyi katika giza,kumbe katikati ya giza lolote maana yake katikati ya mambo tusiyo yaelewa ruhusu yule asiyeonekana ili atoe sauti yake inayoweka ufahamu ndani yetu.Haki sasa pengine umezungukwa na mambo huyafahamu hata sababu zake kwanini yanayokupata na unawaza kwanini wewe.Iwapo wewe ni mkristo wa kweli zingatia hili,Yesu anaongea na wanafunzi wake,watu wale waliotayari kujifunza kwake na kuchukua nira yake na utayari wa kujifunza kwake hata wakati ambao ni wa giza,wakati wa giza ni wakati wa hofu,wakati wa mashaka giza kiafya giza kiuchumi giza pande zote usiruhusu hofu amini uwepo wa Bwana.
     Mungu ana,pokuweka katika giza na unapokuwa pale katika giza funga mdomo wako ili usije ukakamatwa kwa maneno ya kinywa chako “keep your mouth shut”when your in dark.Pengine ndivyo sasa ulivyo upo katika utata wa maisha na maamuzi yako hayaeleweki tulia na jifunze kuto kusemasema ili umuache Mungu aseme,ukifungua kinywa wakati wa giza utaongea vibaya in the wrong mood.Gizani kipindi cha kusikiliza sio kipindi cha kusema,kutokusema sio alama ya kutokujua bali ni adabu ya yeye aonaye gizani,giza halimfichi kitu ukimpa nafasi ukimheshimu na kukaa kimya utamhusisha yeye atamke akitamka neno juu yako neno lake litaumba muujuza wako.Acha kusema na watu juu ya giza lako acha kutafuta sababu za giza kwa wenye hekima na marafiki bali sikiliza Jehova  asemaye katika giza.Ukizungumza na watu hutasikia yale Mungu asemayo utagonganisha maneno ya watu na Mungu na hiyo sio nidhamu ,wewe uwe na nidhamu ya kumsikiliza Mungu  ukiwa katika giza ya yale yakuzungukayo usikivu wako wakati wa giza utakupatia ushuhuda wa thamani sana wakati ukitokea nuruni.Baada a vipindi vya giza huja na vitu mchanganyiko na hofu yenye furaha ndani yake utashangaa mbona ulikuwa huelewi japo ulikuwa unasikia hali hizo,elewa ni majira Mungu ameweka ufahamu na karama ya unyenyekevu unaoleta moyo mnyofu ambao wakati wote utamsikia Mungu asemapo.
        Mungu atuapatie nidhamu ya kusikiliza na kukua katika maarifa ya mapenzi yake pokea ujasiri na usikivu wa Kiungu wakati wa mambo magumu katika jamii,familia,hata Taifa pia tuelewe siku zote sio Jumapili.Tujifunze nidhamu ya kusikiliza wala sio kusema.

              Barikiwa Ev.Yohana Kangajaka Wasiliana nae kwa namba (+225758456221) or +2250715279702 kama ukitaka kusaidia Huduma.Mungu akubariki

Hakuna maoni: