STEWARDSHIP
1Kor 4:1-2 ,Gen 1:1-2
Uwakili ni neno la kivitendo
linatokana na wakili,wakili anapokuwa kazini ule ni uwakili na wakiwa wengi
wanaitwa mawakili(stewards)na maana ya wakili ni mmiliki,ni mwangalizi,ni
msimamizi wa mali ya……….Mwanzo 15:2 sisi kama wana wa Mungu ni watunzaji na
waangalizi wa mali ya Baba yetu,ndio maana Paulo anasema mtu na atuhesabu
hivi,mimi Paulo na Apolo na mitume wengine kama watumishi wa Kristo tu
waangalizi na watunzaji wa mali ya Baba(Men ought to regard us as a servant of
Christ)sisi sio viongozi wa vikundi flani bali wote,popote ni watumishi wa
Kristo,kama kila mmoja angejifahamu namna hiyo kusingekuwa na migawanyiko ndani
ya kanisa maana tumeitwa kila mmoja kama Kiungo cha mwili wa Kristo na kila
mmoja ni wa kipekee(Unique)kwa ajili ya utumishi,wote hatuwi macho(eye)na wote
sio pua na wote sio mikono lakini vyote ni viungo vikitenda kazi kwa ajili ya
mwili kujijenga kwa hiyo wakristo wote
ni watumishi wa kristo,tukijifahamu migawanyiko itakimbia
Mitume wameaminiwa kwa siri za Mungu
siri zilizofichika huwekwa wazi na mitume na manabii,wao ni mkono wa Mungu wa
kufanyia kazi hapa duniani na mkono una vidole vitano Rum 1:17 (Kwa maana haki
ya Mungu inadhihirishwa ndani yake toka imani hata imani kama ilivyoandikwa mwenye
haki wangu ataishi kwa imani) 1wakr 2:7 (Bali twanena hekima ya Mungu katika
siri,ile hekima iliyofichwa ambayo Mungu aliiazimu tangu milele kwa utukufu
wetu,8 ambayo wa kuitawala dunia hii hawaijui hata mmoja maana kama wangaliijua
wasingemshulubisha bwana wa utukufu.9 lakini kama ilivyoandikwa mambo ambayo
jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia wala hayakuiingia katika moyo wa
mwanadamu mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao.10 lakini Mungu
ametufunulia sisi kwa Roho maana Roho huchunguza yote hata mafumbo ya Mungu.11
maana ni nani katika binadamu hayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu
iliyo ndani yake?vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa
Mungu.12 -13)hivyo tunakuwa mawakili wa siri hizo kinachohitajika ni
uaminifu(we must be faithfully katika wajibu tunaopewa Mwanzo
44:1(kasome)Yusuphu alitoa agizo na wasimamizi walilitekeleza kwa sababu ya
uaminifu usio na maswali kwa bosi wao kama wakristo tunapaswa kuwa waaminifu
katika agizo la Mungu wakili mbaya hukutana na mapigo name nataka nikujulishe
siri ya kutoa ziko aina sits za utoaji @Malimbuko(first fruits) b.fungu la
kumi(ten percent) c.Nadhiri(ahadi) d.Dhabihu e.Shukrani f.Sadaka kama mbegu
kila utoaji una Baraka ya kipekee na agizo lake mara nyingi wengi wametoa tu
kama kaini sio kwa kufuata agizo bali walijiongoza wenyewe katika utoaji
matokeo yake sadaka zao zinakataliwa(rejected)Mwanzo 4:3-5,iko Baraka ya ajabu
kwa Yule anayeitikia elekezo la Yehova Yn 6:5-13,kumb 28:1………..,)Hebu tukue
katika imani na kuwa watu wazima,mtu mzima ni Yule anaemtegemea Mungu sana ndio
anaitwa mtu mzima Yn 21:18(Akasema amini,amini nakwambia wakati ulipokuwa
kijana,ulikuwa ukijifunga mwaenyewe na kwenda utakako lakini utakapo kuwa mzee
utainyoosha mikono yako na mwingine atakufunga na kukuchukua usikotaka
Nitakuelezea biblia inavyotuongoza
kufanya Mungu atakacho sio tutakavyo sisi katika utoaji fuatailia katika somo
lijalo ili upate vionjo kamili……………inaendelea
Barikiwa na Ev
Yohana Kangajaka
Imechapiswa na Robert Msele
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni