Aliyemtangulia Bwana
Learn The Holy bible with Ev Yohana Kangajaka (Jifunze Biblia na Ev Yohana Kangajaka)
ALIYEMTANGULIA BWANA
Neno Bwana likiandikwa kwa herufi BWANA linamzungumza
Mungu,Adonai au yahwe ambayo badae walitamka Yehova.Yehova maana yake ni Mungu
muumbaji,yeye aishie kwa uwezo wake mwenyewe,Adonai Bwana mkubwa,akitaka kwenda
mahali wakao marafiki zake anawajulisha wao ndio wanaojua njia atakayopitia
,wanaanda mazingira kuwaweka watu tayari,kumngojea na hivyo kuna watu
wanatangulia,na ving’ora ili kusafisha njia Bwana mkubwa asiweke
foleni,Ving’ora hivyo ndio sauti ya kinabii,na mmoja aliyeitwa sauti ya mtu
aliyae nyikani ambaye alimtangulia Bwana kusafisha njia,jina lake aliitwa
Yohana
Mungu akitaka kufanya jambao lolote kwa mtu,kwa taifa au kwa
dunia lazima awajulishe hiyo siri marafii zake ambao ni manabii,Nabii ni
king’ora cha mbinguni,ni sauti ya mgutusho, Amosi 3:7 (Hakika Bwana Mungu
hatafanya neno lolote,bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake.) Kwa
hiyo Yohana alikuwa rafiki wa Mungu maana nabii ni rafiki wa Mungu,ni mkalimani
wa kile Mungu asimacho,kuwaanda watu waweze kuruhusu uwepo wake.Yohana
aliwaagiza watu wote watubu bila kujali walikuwa watu gani,wa cheo gani,wa dini
gani maadamu ni mtu alipaswa kutubu,kwa sababu Mungu hana upendeleo,njia yake
anayopitia akitaka kufanya kitu ni mioyo ya watu wenye toba,hebu jifunze kuheshimu
sauti za kinabiii badala ya kupambana ingia katika Toba ili Bwana akuandae
kumruhusu Bwana mkubwa Isaya 57:15 (Maana yeye aliyejuu,aliyetukuka,akaaye
milele;ambaye jina lake ni mtakatifu asema hivi,nakaa mimi mahali palipo
inuka,palipo patakatifu,tena pamoja na yeye aliye na roho iliyotubu na
kunyenyekea,ili kuzifufua roho za wanyenyekevu,na kufufua mioyo yao waliotubu.)
Hebu jinyenyekeshe na uwe na toba ya kwelikweli,ghahiri njia
zako mbaya uache uovu wako ili uwe chombo cha kubeba kusudi la Mungu Mt 3:7 -10
(Hata alipoona wengi miongoni mwa mafarisayo na masudukayo wakiujiaa ubatizo
wake,aliwaambia,Enyi uzao wa nyoka,ni nani aliwaonya ninyi kuikimbia hasira
itakayokuja?,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,)Wakati Mungu alipotaka
kuibadilisha historia ya mwanadamu,alimtuma mjumbe maalumu katika injili ya
luka 1:26 (Mwezi wa sita malaika Gabrieli alitumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa
Galilaya jina lake Nazaret) Ukiona neno malaika maana yake ni mjumbe maalumu
Also via Our page on Facebook
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni