MATHAYO ALIITWA NA BWANA
MATHAYO ALIITWA NA BWANA
Mt 9:9--13(Naye Yesu alipokuwa akipita kutoka huko aliona
mtu ameketi forodhani aitwaye Mathayo,akamwambia,nifuate.Akaondoka akamfuata.10
Ikawa alipoketi nyumbani ale chakula,tazama,watoza ushuru wengi na wenye dhambi
walikuja wakaketi pamoja na Yesu na wanafunzi wake.11 Mafarisayo walipoona hayo
waliwaambia wanafunzi wake,mbona mwalimu wenu anakula na kunywa pamoja na
watoza ushuru na wenye dhambi?12 Naye aliposikia aliwaambia,Wenye afya
hawahitaji tabibu bali walio hawawezi.13 Lakini nendeni,mkajifunze maana yake
maneno haya,nataka rehema wala si sadaka;kwa maana sikuja kuwaita wenye haki
bali wenye dhambi.)
Nifuate akaondoka akamfuata,mzigo wa Yesu na maono yake
yakawa maana ya mathayo.Mathayo ameongezwa katika kundi la wanafunzi wa
Yesu,ameteuliwa naye akaondoka katika mazoea ya dhambi,akamfuata yaani akafanya
yale Yesu afanyayo,hakufuata tabia za watoza ushuru wengine wala tabia za jina
lake la kale.Ndipo alivyoona wema wa Yesu alimualika nyumbani kwake na kumpa
Yesu chakula.Chakula cha Yesu ni kufanya mapenzi ya baba yake,mathayo alialika
watoza ushuru wengine ili wakutane na Yesu alijua sasa mafanikio anayo Bwana
mpya Bosi wa maisha yake,alitaka marafiki wamwone.
Wakati huo wayahudi walikuwa wandharau sana watoza ushuru
waliwaona kuwa katika taifa lao ni watu wasio na dini,watu wadanganyifu
,walipomwona Yesu yupo pamoja na katika mlo wakamdharau na Yesu (Mt 9:10—11)
ukisoma Luka 5:27—30(Baada ya hayo akatoka akaona mtoza ushuru,jina lake
Lawi,ameketi forodhani,………………………………………………………….)Yesu alijibu hoja zao,akawaambia
kama hawa watoza ushuru ni wabaya ndio hasa walaohitaji msaada wake.
Mbingu zilikuwa pamoja na Yesu,Mungu Baba alipendezwa na
Tendo la Pendo na neema kwa watu waliotengwa na ushirika wa jamii.Mungu
hapendezwi na sadaka za watu wanaojidai kuwa ni wema kuliko wengine,hebu tambua
thamani yako anayo jehova tu.Acha vyote mfuate utaona utukufu wake nawe utakuwa
chombo,acha dhambi,wengi watanona utukufu wake.Amina
ENDELEA KUFUATILIA HABARI MBALIMBALI KWENYE BLOG YETU UPATE KISA CHA MALKIA WA KUZIMU ALIVYOTAKA KUMSHAMBULIA MTUMISHI WA MUNGU YOHANA KANGAJAKA NA UELEWE JINSI GANI WANAFANYA KAZI ZAO KUPINGA KAZI ZA MUNGU
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni