“IMANI IOKOAYO IMANI IKOMBOAYO NI NINI?”
Yakobo 2:14 “Ndugu
zangu,yafaa nini,mtu akisema kwamba anayo imani,lakini hana matendo?je!ile
imani yaweza kumwokoa?” ile imani;
neno hili ile imani lina maana ni aina gani ya imani inayookoa.Sio kukubaliana
kwa akili na kweli ya biblia kuhusu Mungu Yakobo 2:19 “Wewe waamini ya kuwa
Mungu ni mmoja;watenda vyema.Mashetani nao waamini na kutetemeka” Imani iokoayo
hutenda na kutii.Uwe na upendo wa amri za Mungu na utii Yakobo 2:20 “Lakini
wataka kujua,wewe mwanadamu usiye kitu,kwamba imani pasipo matendo haizai?” Rum
10:9—10 (9.Kwa sababu ukimkiri Yesu kwa kinywa chako kwa kuwa ni Bwana,na
kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu,utaokoka 10.Kwa maana
kwa moyo mtu uamini hata kupata haki,na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu)
Imani humtii Mungu
kwa moyo usio kichwa ?” Rum 10: “Kwa
maana kwa moyo mtu uamini hata kupata haki,na kwa kinywa hukiri hata kupata
wokovu” Efeso 2:8—9,Rum 16:26 (Ikadhihirishwa wakti huu kwa mandiko ya
manabii,itajulikana na mataifa yote kama alivyoamuru Mungu wa milele ili waitii imani) Efeso 2:10
“Maana tu kazi yake,tuliumbwa katika Kristo Yesu,tutende matendo mema,ambayo
tokea awali Mun gu aliyatengeneza ili tuenende nayo” Imani iokoayo ni kipawa
cha Mungu.(Isaya 61:10)ni kuvikwa na kufunikwa (Isaya 64:6,Luka 43:48.Ebra
7:22,Ebra 6:6,Ebra 12:24,Ebra 4:10)sasa yapo maagano na mikataba
Agono na mkataba sio
kitu kimoja kama watu wanavyodhani,Mkataba ni kazi ya binadamu na Agano ni kazi
ya Jehova 1 Yoh 1:8—9 “Tukisema kwamba hatuna dhambi,tunajidanganya
wenyewe,wala kweli haimo mwetu 9.Tukiziungama dhambi zetu,yey ni mwaminifu na
wa haki hata atuondolee dhambie zetu,yeye hutasafisha na udhalimu wote”lazima
tuanze kwa toba iwapo tunataka ukombozi wa kweli Lawi 17:11 “kwa kuwa uhai wa
Mwili u katika hiyo damu;nami nimewapa ninyi hiyo damu juu ya madhabahu,ili
kufany upatanisho kwa ajili ya nafsi zenu;kwani ni hiyo damu ifanyayo
upatanisho kwa sababu ya nafsi” kiri damu ya Yesu 1 Yn 1:7 “Bali tukienenda nuruni,kama alivyo
katika nuru,twashirikiana sisi kwa sisi na damu yake Yesu,mwana
wake,yatusafisha dhambi yote” Ulinzi Kumb 28:7 “Bwana atawafanya adui zako
wainukao juu yako kupigwa mbele yak;watakutokea kwa njia moja,lakini watakimbia
mbele yako kwa njia saba”( 1kor 2:10) Roho (Rum 8:26 “) Kusamehe (Mt 6:14)
Kisasi (Yer 15:15) Uponyaji (Zab 107:20)kukanyaga nguvu za adui.Angusha ngome(
Yoshua 6:20)
Ni hakika kwamba
tumetoka katika jamii tofauti zilizo chini ya maagano mbalimbali ambayo
yamevuta laana mbalimbali sasa kabla ya kuendelea sana ni vyema tuone na kujua
laana maana yake ni nini?LAANA ni maneno yaliyozungumzwa au kunuizwa yenye
uwezo katika ulimwengu wa roho ya kuharibu hatima ya mtu au ukoo na katika
laana hizi zipo aina saba za laana
1. Kuna laana ya Mungu
2. Kuna laana ya Manabii
3. Kuna laana ya Torati
4. Kuna laana ya shetani
5. Kuna laana ya ukoo
6. Kuna laana ya kujifanyia
7. Kuna laana ya kushirikishwa
Na hizo zote zina
nguvu ya kuharibu japo laana ya Mungu ni ngumu sana na laana ya manabii kuliko
laana ya shetani na torati (sheria) ni budi mtu atakaye kutoka katika laana au
anayetaka ukombozi katika laana kwanza awe na imani ikomboayo Biblia inatuambia
katika Rum 1:17 “Kwa maana haki ya Mungu inadhihirishwa ndani yake,toka Imani
hata imani,kama ilivyoandikwa,mwenye haki ataishi kwa Imani” Hivyo tunatoka
Imani hadi Imani,Ushindi hadi Ushindi kwa Ushindi wa Yesu. 1 Kor 15:57 “Lakini Mungu na ashukuriwe
atupae kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo” iyo safari ya kutoka katika laana
na kuingia katika Baraka inaanzia katika ushindi wa Imani (Gal 3:14—15) hatuna
hofu tena wla mashaka yeyote katika Agano alilotupatia Mungu nalo linajengwa
katika uaminifu katika kutii Imani Rum
16:26
Hapo kukwatishwa
tamaa na adui kwa vikwazo anavyoweka katika njia zetu sio mambo yanayoweza
kujenga maisha yenye nguvu na ushindi.Sisi tumepata msaada ulioshuka toka juu.Ushindi
wa Yesu ndio tumepewa yeye aliyekubali kuwa laana,hapa lazima uwe makini laana
inayoongoza kuondoka baada ya mtu kuingizwa katika familia ya Mungu ni ile ya
Torati (Gal 3:13 “Kristo alitukomboa katika laana ya torati,kwa kuwa alifanywa
laana kwaajili yetu;maana imeandikwa ,Amelaaniwakila mtu aangikwaye juu ya
mti.)Ibilisi hana uwezo tena wakuwashinda wala kuwadanganya watu wa
Mungu.(yohana 1:12 Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa
Mungu,ndio wale waliaminio jina lake;) Hapo ndipo wote waliompokea wana kuwa
baba na kupewa uwezo,mamlaka,ruksa,haki(exsosia).Ibilisi anawadanganya wale tu wasio jua wao niwakina nani katika kristo
Yesu.Ushindi wa Yesu ufufuo wa Yesu tumepewa tumehesabiwa haki ya
kuaushindi wetu kwa imani katika neema
yake (yohana 8:32 tena mtaifahamu kweli,nayo hiyo kweli itawaweka huru. Katka
ms 36 basi mwana akiwaweka huru mtakuwa huru kweli kweli.
Tumewekwa huru mbali
na misri na uovu wake,na mizigo yake (Ebr 2:14-15 Basi,kwa kuwa watoto
wameshiriki damu na mwili,yeye naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo,ili
kwanjia ya mauti amharibu yeye aliekuwa na nguvu za mauti,yaani,Ibilisi,awaache
huru wale ambao kwamba maisha yao yote kwa hofu ya mauti walikuwa katika hali
ya utumwa.)Ibilisi ameharibiwa hii sio kwamba hayupo.Hayupo lakini amenyanganywa mamlaka yote na Yesu ndiye anayo
sasa .Yeye alie ushindi wa kifo,neno lililotumika kuharibu kwakiyunani linaitwa
katargeo likiwa na maana ya kusababisha
kutokuwa na uwezo,kutokuwa na umuhimu,kupoozesha.hivyo kwa kupitia kifo cha
Yesu.
Sio kwamba amelipa
adhabu ya dhambi tu bali alimfanya shetani
kutokuwa na uwezo,amemtiisha hadi kukosa nguvu amempoozesha kwahiyo
ukimpokea Yesu huna haja ya kumuogopa ibilisi wala hukumu inayofuata baada ya
kifo wala huogopi wachawi na kundi lake lote la giza. Ebrania9:27 anasema.Na
kama vile watu walivyowekewa kufa mara
moja, na baada ya kufa hukumu. Ebr.10:27 bali kuna kuitazamia hukumu yenye
kutisha,na ukali wa moto uliotayari kuwala wao wapingao Rumi8:1-2 Sasa basi
hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.Kwasababu sheria ya
Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru,mbali na sheria ya
dhambi na mauti.Hapo ndipo mauti
ilipopoteza uchungu wake,usiogope matokeo ya kifo maana hakiwezi kuharibu nafsi
na roho ya aliyeokoka Kristo
anamiliki.pamoja na hayo kama hukwenda sawa na elekezo la Neno la MUNGU ndio
inakua mlango wa kuvuta laana ya BWANA.MITHALI 3:33 Laana ya Bwana I katika
nyumba ya waovu bali huibariki maskani ya mwenye haki hebu uwe na ufahamu
sahihi wenye haki ni ni wale walio amini kazi ya Mungu ya ukombozi kwa njia ya
kifo cha Yesu. Gal 2;16 Hali tukijua ya kwamba mwanadamu hahesabiwi haki kwa
matendo ya sheria,bali kwa imaniya Kristo Yesu;sisi tulimwamini Kristo Yesu ili
tuhesabiwe haki kwa imani ya Kristo Yesu,wala si kwamatendo ya sheria;maana kwa
matendo ya sheria hakuna mwenye mwili atakaye hesabiwa haki.ukifikia cheo hicho
laana isiyo na sababu haikupiga. Maana yake ukiruhusu adui kupata sababu laana
yaweza tenda kazi.mithali 26:2 kama shomoro katika kutangatanga kwake, na kama
mbayumbayu katika kuruka kwake .kadhalika laana isiyo nasababu haimpigi mtu. Sasa
fimbo ya enzi anayo Yesu iwapo tutatembea na kuitia Imani {Rum 16:26
Laana aina ya tatu ni
ya watumishi wa Mungu[Manabii] mfano Yoshua
6:26 “Naye Yoshua akawaapisha kiapo wakti ule,akasema,na laaniwe mbele
BWANA mtu Yule atakayeinuka na kuujenga mji huu wa heriko;ataweka msingi wake
kwa kufiliwa na mzaliwa wa kwanza wake,tena atasimamisha malango yake kwa
kufiliwa na motto wake mwanamume aliye mdogo.” Joshua alipowaapisha kiapo wote
waliyoenda kinyume na kiapo kile uharibifu uliwafika [2 samweli 1:21] Daudi
alipokuwa analia aliongea maneno ambayo yanafanya kazi tangu alipoyanena hadi
leo.Elewa Miaka elfu ya Daudi ndio Yesu akaja miaka Elfu mbili tangu Yesu aje
hadi tulip oleo yale maneno bado yana nguvu,milima ya Gibea haina maongeo
imedumu miaka elfu tatu
Inaendeleaaa……………………..
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni