KUBADILISHWA NA TAABU By Yohana Kangajaka
KUBADILISHWA NA TAABU
2 kor 4:17 “Maana dhiki yetu nyepesi iliyo ya muda wa kitambo tu,yatufanyia
utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana”
Dhahabu safi hutokana na
moto,husafishwa na moto.Mungu analengo kwa kila tatizo,yeye hutumia mazingira
kukuza tabia zetu ili kufanana na Kristo.Mazingira ni zaidi ya kusoma biblia
maana unakabiliana na mazingira masaa 24,(Yn 16:33 “hayo nimewaambieni mpate
kuwa amani ndani yangu.ulimwenguni mnayo dhiki;lakini jipeni moyo;mimi
nimeushinda ulimwengu”) hakuna sugu kwa matatizo wala hakuna aliye funikwa
asikutane nayo ( Ayubu 5:7 “Lakini mwanadamu huzaliwa ili apate mashaka,kama
cheche za moto zirukavyo juu.”)mkitatua moja lingine linakuja 1 petro 4:12
Mungu anayatumia matatizo kutusogeza
karibu sana naye na kutukuza kitabia,iwapo unamjua ukipondeka moyo mtaona
wokovu wake,ibada za kweli huja wakati upo katika hali nzito nyakati za
giza.Unapohisi kuachwa mkiwa na maumivu makali na mkamgeukia Mungu sio
kumkimbia hapo sala zake huwa za kweli na mwaminifu kutoka moyoni Mateso ni
mwalimu.Ebra 5:8 (“na,ingawa ni Mwana,alijifunza kutii kwa mateso hayo
yaliyompata;) maisha yakiwa ya raha waweza mtaja na kumfahamu juu juu tu,ukiiga
na kunukuu.Bali katika tabu utamjua na utajifunza.
Mungu angeweza zuia Yusufu atupwe
gerezani,au Danieli asitupwe katika pango la simba,Yeremia katika simo la
matope,Paulo Mungu angezuia asivunjikiwe na jahazi bali aliruhusu kutokea bila
kizuizi na matokea kila mmoja alimsogelea Mugnu kwa karibu zaidi.shida
utulazimisha kumtazama Mungu na kumtegemea Mungu,Uwezijua kwamba unachohitaji
ni Mungu peke yake hadi pale utakapojikuta umebaki na Mungu pekee.bila kujali
chanza,hakuna tatizo linaloweza kukupata bila ruksa ya Mungu.
Mungu uyachuja yote yanayokukuta na kuyatumia kwa ajili ya
mema (Rum 8:28 “Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja
wale wampendao katika kuwapatia mema,yaan, wale walioitwa kwa kusdi lake”)ingawa
na shetani na watu wengine wanakusudia mabaya kwa Mungu anatawala yote,siku
zako zote zimeandikwa katika kalenda ya Mungu kabla hujazaliwa na kila
kinachokutokea kina umuhimu wa kiroho,Mungu husababisha kila kitu kufanya kazi
pamoja kwa ajili ya mema ya wale wampendao Yn 14 :23 “(Yesu
akajibu,akamwambia,mtu akinipenda,atalishika neno langu,na Baba yangu
atampenda;nasi tutakuja kwake,na kufanya makao kwake”) Rum 8:28-29 and we know
that all things work together for good to them that love GOD, to them who are
called according to his purpose. For
whom he did foreknow, he also did predestinate to be conformed to theimage of his
son,that he might be the first born among many brethren. Neno TUNAJUAni alama ya uhakika wa tumaini wakat
wa magumu hutegemei kufikiri chanya bali unafikiri kwa kule kutarajia mema au
kule kutegemea mazuri huu ni uhakika uliojengwa kwenye kweli.kwamba Mungu
anatawala kikamilifu huu ulimwengu na anatupenda akisema tunajua KWAMBA Mungu husababisha.maana yake
kuna mbinu nyuma ya kila kitu kinachoruhusiwa kutokea hata kama adui
amesababisha Mungu anazombinu sio bahati
mbaya yale yatokeayo kwako yuko msanifu nyuma ya jambo.kumbuka sisi tunaweza
kukosea lakini Mungu hakosei.akisema KILA KITU.maana yake mpango wa MUNGU kwa maisha yako anahusisha yote
yanayotokea pamoja na makosa yetu na dhambi na maumivu yetu,magonjwa unayoutana
nayo madeni yetu majanga talaka.vifo vya wapendwa wetu tuwapendao hayo yote
MUNGU aweza leta mema toka mambo yanayoonekana maovu. Alifanya hivi
kalvari.katika uovu na ukatili wao MUNGU AKALETA WOKOVU KWA WOTE WANAOAMINI.
Kufanya kazi pamoja sio kwa kipekee au
kujitegemea,matukio ktk maisha yako yanategemeana katika mchakato mzima wa
kukufanya ufanane na Kristo. Yote yanachonga SHAPEyako.kama vile mtu
anayetengeneza lishe.kuna vichanganyiko vingi.lakini mwisho wa siku kunatokea
msosi wakufaa kwa afya. Mpe MUNGU MAMBO YAKO YOTE MABAYA NA MEMA KATKA MATUKIO YAKO YOTE MLETEE.atayaunganisha
pamoja kua kitu chema nawe utakuwa na ushuhuda. Yote ni kwa ajili ya mema
lakini hainamaana kwamba kila kitu ni chema bali kila kitu hutendeka kwa ajili
ya meea maana MUngu ni mtaalamu wa kutoa mema kutokana na mabaya mfano ukoo wa
Yesu Kristo wanawake wanne Amari,Ruthu,Rahabu,Bethseba.”TAMARI” alimhadaa baba
mkwe wake, Rahabu alikuwa kahaba,Ruthu hakuwa myahudi na laivunja sheria ya
kuolewa na myahudi,Bethseba alitenda uzinzi na Daudi jambo lililoleta mauaji ya
mume wake.
Hizi hazikuwa ni sifa nzuri lakini
mungu alileta mema mema katika mabaya na Yesu akaja toka ukoo wao.Kusudi la
Mungu lani kubwa kuliko matatizo yetu,maumivu yetu na dhoruba “YA WALE
WAMPENDAO MUNGU NA WAMEITWA =Ahadi ya Mungu ni kwa watoto wake tu si kila kitu hufanya kazi pamoja kwa ubaya
kwa wale wanaoishi kumpinga Mungu na kukazana kufuata njia zao,kutokana na leng
lake ni sisi tufanane na mwanae.Kila kitu kitokacho ni kwa kusudi hilo,jenga
tabia ya mfano wa Yesu.Tunachongwa kwa nguvu ili kuondoa makunyanzi yote kwa
nyundo yenye nguvu,atatumia chochote hadi umechongoka ufanane na Yesu mateso
yanaleta subiri Paulo anasema kila tatizo hujenga tabia na misuli ya kiroho na
uadilifu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni