Jumanne, 31 Desemba 2013
Jumatatu, 30 Desemba 2013
Alhamisi, 26 Desemba 2013
Watumishi wa Mungu Yohana Kangajaka, Mchungaji Silas na mkewe pamoja Mchungaji Herbet Mwaimu na mkewe kulia kwa mtumishi Yohana. Mchungaji Herbet Mwaimu ndiye mkurugenzi wa kituo cha kulelea watoto yatima kilichopo mahali hapa Mbalamo Kwamasimba Korogwe ukitaka kuchangia watoto yatima +255655502133 karibu tuhudumie watoto wetu Yakobo 2:14-18 yafaa nini mtu akisema yakwamba anayo imani lakini hana matendo?................
Jumatano, 25 Desemba 2013
MERRY CHRISMASS AND HAPPY NEW YEAR 2014
WISHING YOU HAPPY CHRISMASS (TUNAWATAKIA HERI YA KRISMASI )
LEO NI SIKU YA FURAHA SANA KWA WATU WOTE DUNIANI TUNAWATAKIA HERI YA KRISMASI NA MWAKA MPYA
LEO TUPO KWA MASIMBA KATIKA KITUO CHA KULELEA WATOTO YATIMA MBALAMO..TUKISHEHEREKEA KWA PAMOJA KWA SIFA NA UTUKUFU WA JINA LA YESU
Jumapili, 22 Desemba 2013
Jumamosi, 21 Desemba 2013
SUNDAY SERVICE IN KKKT HANDENI
MHUBIRI EV YOHANA KANGAJAKA AKIHUDUMU KWENYE IBADA KKKT USHARIKA WA HANDENI
PAMOJA MAFUNDI MITAMBO WAKIMWABUDU MUNGU
MAFUNDI MITAMBO MTUMISHI FRANK KANIKI NA RAPHAEL MRISHO PAMOJA WAKIHUDUMU KATIKA IBADA
MCHUNGAJI KIONGOZI WA USHARIKA HUU KWA PAMOJA NA WAUMINI WAKIFUATILIA IBADA ILIYOKUWA INAONGOZWA NA MWIJILISTI MCHOME PAMOJA NA EV YOHANA KANGAJAKA
Ijumaa, 20 Desemba 2013
MIUGIZA KWA JINA LA YESU KWANI MAPEPO YANATII NA WATU WANAFUNGULIWA
NI WAKATI WA HUDUMA YA MAOMBEZI NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU ZIKIFANYA KAZI KWA JINA LA YESU KUPITIA MTUMISHI WAKE HAPA KKKT USHARIKA WA HANDENI KATIKA MKUTANO WA NENO LA MUNGU
JINA LA BWANA LIBARIKIWE KWANI MAPEPO YANATII AMRI KWA JINA LA YESU
WAHUDUMU WAKIMFANYIA HUDUMA MTU ALIYEKUWA AKISUMBULIWA NA MAPEPO ALIYEANGUKA WAKATI WA MAOMBEZI ILIYO KATIKA HUDUMA YA KINABII NA MTUMISHI YOHANA KANGAJAKA
MHUBIRI :GRACE MPANDUJI
KICHWA:TUNASHUGHULIKIA WACHAWI WAPONE
MATENDO YA MITUME 8:9--13
(Na mtu mmoja,jina lake simoni,hapo kwanza alikuwa akifanya uchawikatika mji ule,akiwashangaza watu wa Taifa la wasamaria,akisea yeye ni mtu mkubwa.10 Wote wakamsikiliza tangu mdogo hata mkubwa,wakisema,mtu huyu ni uweza wa Mungu,ule Mkuu.11 Wakamsikiliza,kwa maana amewashangaza muda mwingi kwa uchawi wake.12 Lakini walipomwamini Filipo,akizihubiri habari njema za ufalme wa Mungu,na jina lake Yesu Kristo,wakabatizwa,wanaume na wanawake.Na yeye Simoni mwenyewe aliamini akabatizwa,akashikamana na Filipo;akashangaa alipoziona ishara na miujiza mikubwa inayotendeka)
Alhamisi, 19 Desemba 2013
MATHAYO ALIITWA NA BWANA
MATHAYO ALIITWA NA BWANA
Mt 9:9--13(Naye Yesu alipokuwa akipita kutoka huko aliona mtu ameketi forodhani aitwaye Mathayo,akamwambia,nifuate.Akaondoka akamfuata.10 Ikawa alipoketi nyumbani ale chakula,tazama,watoza ushuru wengi na wenye dhambi walikuja wakaketi pamoja na Yesu na wanafunzi wake.11 Mafarisayo walipoona hayo waliwaambia wanafunzi wake,mbona mwalimu wenu anakula na kunywa pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi?12 Naye aliposikia aliwaambia,Wenye afya hawahitaji tabibu bali walio hawawezi.13 Lakini nendeni,mkajifunze maana yake maneno haya,nataka rehema wala si sadaka;kwa maana sikuja kuwaita wenye haki bali wenye dhambi.)
Nifuate akaondoka akamfuata,mzigo wa Yesu na maono yake yakawa maana ya mathayo.Mathayo ameongezwa katika kundi la wanafunzi wa Yesu,ameteuliwa naye akaondoka katika mazoea ya dhambi,akamfuata yaani akafanya yale Yesu afanyayo,hakufuata tabia za watoza ushuru wengine wala tabia za jina lake la kale.Ndipo alivyoona wema wa Yesu alimualika nyumbani kwake na kumpa Yesu chakula.Chakula cha Yesu ni kufanya mapenzi ya baba yake,mathayo alialika watoza ushuru wengine ili wakutane na Yesu alijua sasa mafanikio anayo Bwana mpya Bosi wa maisha yake,alitaka marafiki wamwone.
Wakati huo wayahudi walikuwa wandharau sana watoza ushuru waliwaona kuwa katika taifa lao ni watu wasio na dini,watu wadanganyifu ,walipomwona Yesu yupo pamoja na katika mlo wakamdharau na Yesu (Mt 9:10—11) ukisoma Luka 5:27—30(Baada ya hayo akatoka akaona mtoza ushuru,jina lake Lawi,ameketi forodhani,………………………………………………………….)Yesu alijibu hoja zao,akawaambia kama hawa watoza ushuru ni wabaya ndio hasa walaohitaji msaada wake.
Mbingu zilikuwa pamoja na Yesu,Mungu Baba alipendezwa na Tendo la Pendo na neema kwa watu waliotengwa na ushirika wa jamii.Mungu hapendezwi na sadaka za watu wanaojidai kuwa ni wema kuliko wengine,hebu tambua thamani yako anayo jehova tu.Acha vyote mfuate utaona utukufu wake nawe utakuwa chombo,acha dhambi,wengi watanona utukufu wake.Amina
ENDELEA KUFUATILIA HABARI MBALIMBALI KWENYE BLOG YETU UPATE KISA CHA MALKIA WA KUZIMU ALIVYOTAKA KUMSHAMBULIA MTUMISHI WA MUNGU YOHANA KANGAJAKA NA UELEWE JINSI GANI WANAFANYA KAZI ZAO KUPINGA KAZI ZA MUNGU
Tunaendelea kuwakaribisha katika Semina tena siku ya leo ndani ya viwanja vya KKKT Usharika wa Handeni
MHUBIRI;GRACE MPANDUJI
SOMO;NYAKATI ZA HATARI
2TIMOTHEO 3:1
(Lakini ufahamu neno hili,ya kuwa siku za mwishokutakuwako nyakati za hatari.2 maana watakuwa wa kujipenda wenyewe,wenye kupenda fedha,wenye kujisifu,wenye kiburi,wenye kutukana,wasiotii wazazi wao,wasio na shukrani,wasio safi.3 wasiowapenda wakwao,wasio taka kufanya suluhu,wasingiziaji,wasiojizuia,wakali,wasiopenda mema.4 Wasaliti,wakaidi,wenye kujivuna,wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu ;5 wenye mfano wa utauwa,lakini wakikana nguvu zake,hao nao jiepushe nao.)
ENDELEA KUFUATILIA KUPITIA YOUTUBE @ http://www.youtube.com/channel/UCNQi8Dm-n98w671gUKbpiew/videos NA FACEBOOK PAGE @https://www.facebook.com/yohana.kangajaka.3
WEBSITES :WWW.KANGAJAKA.COM
NYAKATI ZA HATARI
Tunaendelea kuwakaribisha katika Semina tena siku ya leo ndani ya viwanja vya KKKT Usharika wa Handeni
MHUBIRI;GRACE MPANDUJI
SOMO;NYAKATI ZA HATARI
2TIMOTHEO 3:1
(Lakini ufahamu neno hili,ya kuwa siku za mwishokutakuwako nyakati za hatari.2 maana watakuwa wa kujipenda wenyewe,wenye kupenda fedha,wenye kujisifu,wenye kiburi,wenye kutukana,wasiotii wazazi wao,wasio na shukrani,wasio safi.3 wasiowapenda wakwao,wasio taka kufanya suluhu,wasingiziaji,wasiojizuia,wakali,wasiopenda mema.4 Wasaliti,wakaidi,wenye kujivuna,wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu ;5 wenye mfano wa utauwa,lakini wakikana nguvu zake,hao nao jiepushe nao.)
Jumatano, 18 Desemba 2013
Mtumishi wa Mungu Grace Mpanduji akihubiri wakati wa Mkutano wa Injili KKKT usharika wa Handeni
TUNAENDELEA KUWAKARIBISHA KATIKA MKUTANO WA INJILI UNAONDELEA HAPA KATIKA VIWANJA VYA KKKT USHARIKA WA HANDENI
MHUBIRI:GRACE MPANDUJI
SOMO:ZABURI 121
KUZUNGUMZA NA MILIMA
ZABURI;121 (Nitayainua macho yangnu kutazama milima,msaada wangu utatoka wapi?2 Msaada wangu u katika BWANA,Aliyezifanya mbingu na nchi.3 Asiuache mguu wako usogezwe;Asisinzie akulindaye;4 Naam hatasinzia wala hatalala usingizi,Yeye mlinzi wa Israeli.5 Bwana ndiye Mlinzi wako;Bwana ni uvuli wa mkono wako wa kuume.6 Jua halitakupiga mchana,wala mwezi wakati wa usiku.7 Bwana atakulinda na mbaya yote,atakulinda nafsi yako.8 Bwana atakulinda utokapo na uingiapo,Tangu sasa na hata milele
Jumanne, 17 Desemba 2013
Mtumishi Akitoa Mfano wa Kitu katika Mkutano wa Injili KKKT Usharika wa Handeni
Alitoa mfano jinsi gani tunajiweka tukiwa duniani ya kwamba tunakaa kama ndo tumefika nyumbani kwetu na kuweka miguu juu wakati sisi ni wageni tu katika hii dunia na tunatakiwa kukaa wima sio kukaa kwa kujiachia tukidhania ya kwamba tumefika kwetu hivyo ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha ya kwamba anafanikiwa kurudi nyumbani kwa Mungu ijapokuwa lazima kupita katika shida na taabu ila kwa usaidizi wa Yesu Kristo mwenyewe.Tusijitwalie ufalme usiokuwa wa kwetu
Ev Yohana Kangajaka Akihubiri kwenye Mkutano wa Injili KKKT Usharika wa Handeni
SOMO:UFUNUO 21:1(Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya;kwa maana mbingu za kwanza na nchi za kwanza zimesha kupita,wala hapana habari tena.2Nami nikauona mji ule mtakatifu,Yerusalemu mpya,ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu,umewekwa tayari,kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,)
Ev Yohana Kangajaka akiendelea na Mahubiri
KUWA KUTOKA KATIKA UTOTO NA FANYIKA MWANA WA MUNGU
Yn 1:12
Bali wote waliompokeaa aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu.Ndio wale waliaminio jina lake.(Yoshuan)Mkombozi,naye Jehova ataka tukue toka motto tufikie utu uzima.Ziko hatua 3
· Teknion
· Teknon
· Hunioth(luiothesia)
Ebr 5:13-14.(Kwa maana kila mtu atumiaye maziwahajui sana neno la haki,kwa kuwa ni mtoot mchanga.14 lakini chakula kigumu ni cha watu wazima,ambao akili zao,kwa kutukiwa zimezoezwa kupambanua mema na mabaya) Acha kujivunia udhehebu,jivunie mwokozi pekee yake ndiye njia yaw ewe kutoka katika vifungo ndiye kweli,ndiye uzima,Paulo anasema Rum 8:15(Kwa kuwa hamkupokea tena roho ya utumwa iletayo hofu,bali mlipokea roho wa kufanywa wana,ambayo kwa hiyo twalia Aba,yaani Baba) tuwekwa kama wana baba atuamini,,,ukisoma Yn 2:23-25(hata alipokuwa Yerusalemu wakati wa Pasaka,watu wengi waliliamini jina lake………………………………) (Gal 4:1-2)
Exosia=haki,faida,mamlaka mfano Tukimpokea Yesu tunapokea haki ya wana Ebra 4:15,,,,pengine unja haki ya hao warithio ahadi bali kutokuamini kutakukoshesha Ebr 6:12 (ili msiwe wavivu bali mkawe wafuasi wa hao warithio ahadi kwa imani na uvumilivu) na 1kor 3:1-2,7,,,,,,,,,,pevuka urithi ahadi umeahidiwa Exosia ya uana sio udini pevuka ili uwe vile Mungu anavyokusudia uwe,toka horini luka 2:7(Akamzaa mwanawe kifungua mimba,akamvika nguo za kitoto,akamlaza katika hori la kulia ng’ombe,kwa sababu hawakupata nafasi katika vyumba vya wageni)….1Yn 2:12-13 keti katika waalimu luka 3:23(Na Yesu mwenyewe alipoanza kufundisha,alikuwa amepata umri wake kama miaka thelathini,akidhaniwa kuwa ni mwana wa Yusufu,wa Eli)uwekwe kama mwana,sio kumuamini tu bali Bwana kujiaminisha kwako.uwe na uwezo wa kufanya suluhu Mt 3:16…Mbingu zinamfunukia kutoa uzima uponyaji,jua la haki linawaka sasa........
Barikiwa sana kwa kuendelea kufuatili
FOLLOWS US ON @https://www.facebook.com/yohana.kangajaka.
Jumatatu, 16 Desemba 2013
We Fire out in Jesus Name
Ni katika Huduma ya Maombezi kwenye Mkutano wa Injili Mchungaji kiongozi (Kushoto)wa KKKT Usharika wa Handeni pamoja na Mkuu wa Dinari(kulia)wakashirikiana pamoja na watumishi wengine wakati wa Maombezi
We are Worship to Jesus!!Haleluya
Mwongazaji wa Present worship akimwabudu Mungu pamoja na makutano kabla ya kuanza huduma ya maombezi
Ev Yohana kangajaka akihubiri wakati wa mkutano wa injili KKKT Usharika wa handeni
Somo la leo Mwanzo 8:1 (Na Mungu akamkumbuka Nuhu,na kila kilicho hai,na wanyama wote walikuwamo pamoja nae katika safina;Mungu akavumisha upepo juu ya nchi maji yakapungua)
Mkuu wa Dinari pamoja na viongozi wengine wakati wa Ufunguzi wa Mkutano KKKT Usharika wa Handeni
Tunamsifu Mungu
Mkuu wa Dinari pamoja na Mchungaji Kiongozi wakifuatilia mahubiri wakati wa Mkutano huo unaoendelea hapa katika viwanja hivi vya KKKT Usharika wa Handeni
Mkuu wa Dinari pamoja na Mchungaji Kiongozi wakifuatilia mahubiri wakati wa Mkutano huo unaoendelea hapa katika viwanja hivi vya KKKT Usharika wa Handeni
Jumapili, 15 Desemba 2013
Aliyemtangulia Bwana
Learn The Holy bible with Ev Yohana Kangajaka (Jifunze Biblia na Ev Yohana Kangajaka)
ALIYEMTANGULIA BWANA
Neno Bwana likiandikwa kwa herufi BWANA linamzungumza Mungu,Adonai au yahwe ambayo badae walitamka Yehova.Yehova maana yake ni Mungu muumbaji,yeye aishie kwa uwezo wake mwenyewe,Adonai Bwana mkubwa,akitaka kwenda mahali wakao marafiki zake anawajulisha wao ndio wanaojua njia atakayopitia ,wanaanda mazingira kuwaweka watu tayari,kumngojea na hivyo kuna watu wanatangulia,na ving’ora ili kusafisha njia Bwana mkubwa asiweke foleni,Ving’ora hivyo ndio sauti ya kinabii,na mmoja aliyeitwa sauti ya mtu aliyae nyikani ambaye alimtangulia Bwana kusafisha njia,jina lake aliitwa Yohana
Mungu akitaka kufanya jambao lolote kwa mtu,kwa taifa au kwa dunia lazima awajulishe hiyo siri marafii zake ambao ni manabii,Nabii ni king’ora cha mbinguni,ni sauti ya mgutusho, Amosi 3:7 (Hakika Bwana Mungu hatafanya neno lolote,bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake.) Kwa hiyo Yohana alikuwa rafiki wa Mungu maana nabii ni rafiki wa Mungu,ni mkalimani wa kile Mungu asimacho,kuwaanda watu waweze kuruhusu uwepo wake.Yohana aliwaagiza watu wote watubu bila kujali walikuwa watu gani,wa cheo gani,wa dini gani maadamu ni mtu alipaswa kutubu,kwa sababu Mungu hana upendeleo,njia yake anayopitia akitaka kufanya kitu ni mioyo ya watu wenye toba,hebu jifunze kuheshimu sauti za kinabiii badala ya kupambana ingia katika Toba ili Bwana akuandae kumruhusu Bwana mkubwa Isaya 57:15 (Maana yeye aliyejuu,aliyetukuka,akaaye milele;ambaye jina lake ni mtakatifu asema hivi,nakaa mimi mahali palipo inuka,palipo patakatifu,tena pamoja na yeye aliye na roho iliyotubu na kunyenyekea,ili kuzifufua roho za wanyenyekevu,na kufufua mioyo yao waliotubu.)
Hebu jinyenyekeshe na uwe na toba ya kwelikweli,ghahiri njia zako mbaya uache uovu wako ili uwe chombo cha kubeba kusudi la Mungu Mt 3:7 -10 (Hata alipoona wengi miongoni mwa mafarisayo na masudukayo wakiujiaa ubatizo wake,aliwaambia,Enyi uzao wa nyoka,ni nani aliwaonya ninyi kuikimbia hasira itakayokuja?,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,)Wakati Mungu alipotaka kuibadilisha historia ya mwanadamu,alimtuma mjumbe maalumu katika injili ya luka 1:26 (Mwezi wa sita malaika Gabrieli alitumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa Galilaya jina lake Nazaret) Ukiona neno malaika maana yake ni mjumbe maalumu
Endelea kufuatilia pia mafundisho mbalimbali kupia Youtube @http://www.youtube.com/my_videos?o=U
Also via Our page on Facebook
Mchungaji Kiongozi akifungua Mkutano pamoja na Mkuu wa Dinari unaoanza Leo na kuisha Siku ya Jumapili ijayo
Neno la Ufunguzi wa Mkutano linatoka Luka 1:26 (Mwezi wa sita,Malaika Gabrieli alitumwa kwenda mpaka Mji wa galilaya jina lake nazareth.,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,)
Mchungaji Kiongozi Leus Shemkala wa Kanisa la KKKT Usharika wa Handeni,akikaribisha makutano pamoja na wageni mbalimbali waliohudhuria Mkutano.Jina la Bwana libarikiwe
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)